Upendeleo Yanga unaishusha hadhi TFF

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Yanga ndiyo klabu kongwe zaidi inayoshiriki ligi kuu nchini. Klabu hiyo ya Jangwani ilianzishwa 1935. Kutokana na ukubwa na umri wake, NIPASHE tulitarajia kuona klabu hiyo inakuwa mfano wa kuigwa na klabu nyingine changa, lakini imekuwa kinyume chake.

Katika siku za karibuni tumeshuhudia Yanga ikiwa mstari wa mbele katika kukiuka misingi, taratibu na kanuni za uendeshaji wa soka ikiwamo katiba ya klabu hiyo.

Hata hivyo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeshindwa kuchukua hatua stahiki dhidi ya Yanga licha ya klabu hiyo kukiuka katiba ya shirikisho hilo kwa kutoitisha mkutano mkuu wa uchaguzi.


Mara ya mwisho Yanga ilifanya uchaguzi mkuu wake Julai 18, 2010. Waliochaguliwa katika uchaguzi huo walikuwa Lloyd Nchunga (mwenyekiti) na Davis Mosha (makamu mwenyekiti) wakati wajumbe waliochaguliwa walikuwa Charles Mgondo, Ally Mayay, Mzee Yusuf, Theonest Rutashobolwa, Titus Ossoro, Sara Ramadhani, Mohamed Binda na Salum Rupia.

Uongozi huo ulikumbwa na changamoto ya baadhi ya viongozi kujiuzulu nyadhifa zao na hivyo ikalazimika kufanyika mkutano mkuu wa dharura wa uchaguzi wa viongozi wa muda Julai 15, 2012, uchaguzi uliowaweka madarakani viongozi waliopo sasa.

Muda wa viongozi hao kukaa madarakani ulioanzia Julai 18, 2010, ulifikia kikomo Julai 17, 2014, lakini Juni Mosi mwaka jana wanachama wa klabu hiyo waliokutana jijini Dar es Salaam waliwaongeza mwaka mmoja kwa maelezo kwamba mkutano mkuu wa uchaguzi wa Yanga ungelifanyika Juni mwaka huu.

Huku kukionekana kutokuwapo kwa dalili yoyote ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Yanga kwa sasa, TFF iko kimya kuhusu suala hilo. Watendaji wa shirikisho hilo wako mstari wa mbele kuingilia masuala ya kiuongozi katika klabu nyingine za soka nchini.

Kwa sasa shirikisho hilo linaisimamia klabu ya Coastal Union ya Tanga kuhakikisha inafanya uchaguzi wa viongozi. TFF pia imeingilia mgogoro wa kiungozi ulioikumba klabu ya Toto Africans ya Mwanza.

Upendeleo wa wazi kwa Yanga ulifanywa na TFF katika msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya shirikisho hilo kutochukua hatua dhidi ya nyota kadhaa wa Yanga waliofanya makosa ya kinidhamu.

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' alimdhalilisha kwa kumkumbatia na kumpiga mabusu askari polisi mwanamke aliyekuwa na sare za Jeshi la Polisi Tanzania alipoifungia timu yake bao pekee la ushindi dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Februari 4, lakini TFF haijachukua hatua zozote dhidi yake.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Amissi Tambwe, alimdhalilisha kwa kumvuta katikati ya miguu beki wa kati wa Simba, Mganda Juuko Murshid, katika mechi ya watani kwenye Uwanja wa Taifa Machi 8, lakini TFF bado haijamwadhibu Mrundi huyo licha ya kukiuka Ibara ya 11(f) cha Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.

Wakati nyota hao wawili wakifumbiwa macho na TFF, tulishuhudia msimu uliopita Kamati ya Nidhamu ya shirikisho hilo ikichukua hatua dhidi ya wachezaji na makocha wa klabu nyingine zikiwamo Azam, Mbeya City, Kagera Sugar, Police Moro na Ndanda FC.

Hiyo ni mifano michache ambayo NIPASHE tunaona jinsi shirikisho linavyojishusha hadhi kwa kushindwa kuchukua uamuzi stahiki dhidi ya baadhi ya klabu za soka nchini.

Kuitisha mkutano mkuu wa uchaguzi (kwa klabu zinazomilikiwa na wanachama ikiwamo Yanga) ni jambo la kikatiba ambalo halina mjadala.

Tunaamini ni wakati mwafaka kwa TFF kuwasimamia wanachama wake, ikiwamo klabu ya Yanga kufanya chaguzi zitakazotoa viongozi wanaochaguliwa kwa utashi wa wanachama wa klabu husika na si vinginevyo.

NIPASHE tunaamini kuwa kitendo cha TFF kufumbia macho mabaya na ukiukwaji wa katiba unaofanyika katika klabu ya Yanga, kunashusha hadhi ya mamlaka hiyo ya juu kisoka nchini.

Kwa kutambua umuhimu wa mamlaka hii katika uendeshaji wa soka nchini, tunatumia fursa hii kuushauri uongozi wa TFF kujikita katika misingi ya kiuweledi katika kuendesha shughuli za mpira wa miguu nchini badala ya kuwa na upendeleo kwa baadhi ya watu na klabu kama inavyoonekana kwa sasa.

Chanzo: Nipashe
 
Nipashe ni IPP nayo inamilikiwa na Mengi huyu mmiliki ana bifu na Manji kisa Yanga....
 
MANJI vs MENGI ....TAHADHARI....yanga ipo vizuri kwa sasa tafadhali msichokonoe mengine.
 
Na kale kisheria ka kuchagua mechi za Kucheza baada ya kupata kadi za njano kaliipendelea Yanga bila shaka. Naona mwandishi kasahau hilo.
Sheria yenyewe imefutwa baada ya kutimiza malengo yake. Yanga oyee!
 
Kweli nimehamini maneno ya Mwenyekiti Manji huyu mengi kuna kitu anakitafuta Yanga
 
Rais nchi Yanga,rais Wa tff yanga,makamu wa rais tff yanga,rais wa cecafa yanga,Kocha wa taifa stars yanga,nahodha wa taifa stars yanga,nahodha wa Rwanda yanga,nahodha wa Zanzibar heroes yanga,nahodha Wa stars maboresho yanga.Ni yanga tu nchi hii.
 
Rais nchi Yanga,rais Wa tff yanga,makamu wa rais tff yanga,rais wa cecafa yanga,Kocha wa taifa stars yanga,nahodha wa taifa stars yanga,nahodha wa Rwanda yanga,nahodha wa Zanzibar heroes yanga,nahodha Wa stars maboresho yanga.Ni yanga tu nchi hii.

Ni kama maji usipokunywa utaoga/kufulia/kuoshea vyombo haiepukiki ndo mana unaambiwa ni timu ya kimataifa
 
hata brazil inapendelewa na FIFA,wacha ujinga wewe hilo ni bifu la mengi na manji
 
mikia wakichagua mechi za kucheza wakati okwwiii ana kadi 3 za njano tuliuliza? mbona klabu zingine hazikufanya hivyo?
 
Mtu mwenye akili timamu hawezi kufuatilia mpira wa Tanzania kamwe. Yanga timu ya kuigwa kwa vigezo gani, mpira wenyewe hawajuwi kucheza zaidi ya kurogana.
 
huyu mengi anafikiri anavyoichezea serikali aje kuichezea yanga shauri yake
 
Mtu mwenye akili timamu hawezi kufuatilia mpira wa Tanzania kamwe. Yanga timu ya kuigwa kwa vigezo gani, mpira wenyewe hawajuwi kucheza zaidi ya kurogana.

Kwa hiyo wewe mwenye akili timamu unafuatilia ligi ya nchi gani?
 
rais wanchi yanga,naibu wazr wamichezo yanga,raic wa cecafa yanga,rais wa tff yanga makamu wake yanga,kocha wa stars yanga msaidz yanga,captein stars yanga wa zanzbar heros yanga na stars maboresho yanga,mchezaji bora wa lig yanga.TUTAPONA KWELI JAMANI?
 
Naibu waziri wa michezo nkamia ni mkia damu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…