Upendo hauombwi Kuomba upendwe ni ubinafsi

Upendo hauombwi Kuomba upendwe ni ubinafsi

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Umekuwa omba omba wa upendo, unahitaji mtu wa kukupa upendo lakini upendo wenyewe ni asili

Unaye muomba upendo kosa huanza hujui ni namna gani anajipenda, nikweli ana upendo lakini hufahamu muendeleo wa upendo ndani yake

Kuna wakati unaomba upendo kwa watu wanao jichukia zaidi na kuonesha kuwa hawajichukii,wanakupa upendo

Lakini hawakupi upendo kwa muendeleo bali kwa muundo, muundo pekee hutoa upendo batili

Wewe ni ombaomba unasimama mbele ya ombaomba mwingine ukiwa na bakuli la kuomba upendo.

Kila ombaomba wa upendo ni mbinafsi.Anajitazama yeye anahitaji kupendwa kwa namna ya taswira yake yeye tu

Kwasababu ya ombaomba ndoa zenye sumu hutokea, mahusiano ya kupeana faraja hutokea

Lakini yote yapo katika muundo,kwa maana ombaomba wote wanahitaji kupendwa kama sehemu ya malipo

Mnanjaa ya upendo kwasababu mna mioyo mikavu iliyo tupu,kila mmoja anafikiri yeye ana stahili kupendwa

Mnakinahiana haraka pale ombaomba wawili mnapokuwa katika maskani ya kuomba kwa sababu matarajio yenj ni makubwa kuliko muendeleo

Omba omba huhitaji kupendwa kwa huruma,hutoa upendo wa huruma hivyo ni dhaifu wanao tembea katika mwendo wa upofu

Huruma si njia ya kuupata upendo kihisia ,usiitoe ili upate upendo lakini unaweza kutoa ili upate ngono kwakua ni ombaomba

Naomba unioe,naomba unipende sana, nitapata nani wa kunipenda naomba nipate Mtu sahihi wa kuwa nae katika upendo, wewe ni sahihi?bado una upendo wa gizani

Utadanganywa,utasalitiwa na utaona yakuwa si mtu unaye stahili kuwa naye hata hilo si tatizo ila tatizo ni omba omba wa upendo ndiyo maana umejikuta huko
 
Back
Top Bottom