Wakati mwingine ndio kuwa na baba ambae ni mzee kijana. Baba huyo hajali kama kijana wake amerudi ama amelala, matoke yake ndio hayo mzazi ana-assume kuwa kila kitu kiko ok. Lakini mzazi responsible anaekaa na mwanae ikipita 24 hrs bila kumwona basi lazima antenna zitasimama kichwani na ataanza kumwuulizia. huyu baba ni mzembe na anatakiwa na polisi awe the person of interest in this case.
Dunita siku hizi ni tafran tu
believe me you, siku hizi watu wanaishi kama wanyama! kuna wanandoa wanaishi hivi! kama mtu mkewe/mumewe anaweza kuwa safari na hawajuliani hali siku 5, na mtu yuko 100kms away! seuze baba na amwana? na ukiwakuta na majirani ama coaligues wanavyokenua meno,huwezi amini kaacha maiti ndani! nimekumbuka uzi wa pdiddy kuhusu wanandoa kusalimiana asubuhi. next tutashuhudia wanandoa, na ndoa zetu za kuuzia sura hizi! so sad! it cant be emphasised jamani, mimi without my very extended family,i am nothing! hata nipewe hela za jairo na change za gen shimbo, i will still feel a huge gap in my heart!
King.. that is what i mean... kua jamani siamini kua we are that busy kua mtu wa familia moja msionane... Mfano mzuri ni kua waweza kua na shughuli inakutoa ndani alfajiri saana wakati woote wamelala... But ni muhimu ukagonga milango na kuita walau usikie sauti na uage hata kama hamjaonana but sound inaonesha the person yupo good. Yaani nyumba moja nisionane na mtu the whole day?? hata kama nimerudi saa sita usiku lazima nimgongee nimsemeshe hata mlangoni walau kujua kua yupo ok... Tukiendekeza haya mambo ya kua busy... tutavunja morals kabisa... Mbaya saana.
kweli kabisa, yaani hata walau simu? ni ustaarabu kusalimia wa nyumbani kwako kabla ya kutoka. hata kama mtoto ni teja ama chizi, kumjali ni muhimu sana! na hata ikiwezekana mchana mwingi kujuliana hali nayo inapendeza! inasikitisha, eti tuko busy! to busy to enjoy what life has to offer!
Kama mzazi si kipenzi cha familia yake na wala si mtu mwenye kupendwa katika familia yake, vipi anaweza kuwa mtu bora katika jamii inayo mzunguka, wakati hata familia ya watu wanne inamshinda kuiongoza?
Wengi hawajui kuwa Familia ni taasisi yenye mchango muhimu mno katika ujenzi wa jamii bora ya wanadamu. Taasisi hii ikishindwa kutimiza wajibu wake, jamii huwa jaa la maasi, kila mwenye uchafu wake huutupia humo... Huyo baba sidhani kama ni mtu wa dini kweli... na hata huo ushirikiano wake mzuri na watu ni wa kinafiki...! Kama ameshindwa kuchunga nyumba yake, vipi anaweza kuichunga jamii inayo mzunguka?
Unajuwa mzazi kadiri anavyotumia wakati wake kuwa pamoja na watoto wake, anakuwa na uwezo zaidi wa hisia ya kugundua kitu gani kinawakera na si kuziswaga hisia hizo chini ya ufungu (usiufiche ukweli). Kuongea kwa uwazi. Lakini si kwenye mikutano ya kifamilia au mbele ya wengine. Kufanya hivyo kutawafanya watoto na wazazi wao kuwa karibu sana.Hayo maneno umetoa... ni ya msingi saaana... na kwa kuongezea ni kua kuendeleza familia... it takes extra effort ili kuhakikisha all that is crucial kwa familia nzima iko provided plus UPENDO hapo hapo...
Unajuwa mzazi kadiri anavyotumia wakati wake kuwa pamoja na watoto wake, anakuwa na uwezo zaidi wa hisia ya kugundua kitu gani kinawakera na si kuziswaga hisia hizo chini ya ufungu (usiufiche ukweli). Kuongea kwa uwazi. Lakini si kwenye mikutano ya kifamilia au mbele ya wengine. Kufanya hivyo kutawafanya watoto na wazazi wao kuwa karibu sana.
Maana watoto wakishafika umri wa kujitegemea wanapaswa nao kuheshimiwa na kujadiliana nao kiutu uzima, japokuwa wazazi wengi hawataki kuwaona watoto wao kuwa wameshakuwa watu wazima na wenye fikra zao.
Ni kweli huyasemayo, wazazi wengi upenda kuwaona watoto wao wakifanikiwa na wakiwa na maisha bora, lakini ni wazazi wangapi tumewaona au kushuhudia wakiwapinga watoto wao kuhusiana na wapenzi wao na kutaka kuoa wale wanao wataka wao...! Wakati mwingine kesi huwa kubwa mpaka kuto tembeleana!?X-PASTER hapo kwenye red i beg to differ, kusema kweli ni raha iliyoje kumlea mwanao akafikia hatua ya kujitegemea,akaweza kupanga chumba chake,akaweza siku moja moja akawapa ka vocha wadogo zake,akatafuta siku baba/mama twende nikakuonyeshe kiwanja nilichonunua,ni jambo la fahari sana.na ndo maana wazazi tunahangaika kusomesha ili vijana wetu wafikie hatua ya kujitegemea sio ki uchumi tu lakini hata kimawazo,sio kila kitu 'ngoja nikamuulize baba' au 'ngoja nikamuulize mama'.
kuhusu uzi wa Asha,inasikitisha sana,mi nashauri tu mzazi kama una watoto jenga utamaduni wa kusalimiana nao kila asubuhi,bora msalimiane anayebaki nyumbani basi arudi kulala kama anataka.