Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Wanaotufundisha umuhimu wa upendo, kadiri ya maagizo ya kitabu Kitakatifu cha Biblia, wanatuambia kuwa, Umpende mwenzako kama unavyojipenda mwenyewe. Sijawahi kuona wala kusikia kuwa kuna mahali imenenwa umpende mwenzako zaidi ya unavyojipenda mwenyewe. Na Mungu pekee yake ndiye aliupenda sana ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili ulimwengu upone. Kwa mwanadamu, ni vigumu sana.
Napenda niamini maneno ya Mbarawa na wale wote wanaomwunga mkono kuwa mkataba wa bandari kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai, ndio mkataba mzuri kuliko yote ambayo tunayo, na kwamba DP ikishachukua bandari zote za Tanganyila:
1) Itakuwa mwisho wa tatizo la ajira kwa vijana wa Tanzania
2) Zaidi ya 60% ya bajeti itachangiwa na mapato ya bandari pekee. Na hivyo kwa sababu bajeti yetu 40% huwa inajazilizwa na misaada na mikopo. Kodi zetu zote toka viwandani, kwa wafanyakazi, wafanyabiashara, tozo, migodi, utalii, adhabu za barabarani, ushuru wa mazao na misitu huwa zinachangia 60%. Hii ina maana kutokana na ujio wa DP, bwana Mbarawa anataka kusema sasa tunaweza kufuta kodi, tozo na ushuru wote, na pengo likazibwa na DP pekee yake, halafu 40% iliyosalia tukaendelea kujazilizia kwa mikopo na misaada. Watanganyika wataishi bila ya bugdha ya kodi, tozo wala ushuru. Tanganyika itaingia kwenye orodha ya zile nchi chache sana Duniani ambazo wananchi wake hawalipi kodi yoyote! Neema kubwa hii toka DP iliyosababishwa na upendo wa pekee wa bwana Mbarawa na katibu wake Aisha Amour, wote wazanzibari.
Mahali panaposhangaza zaidi, Mbarawa na Amour, wote wazanzibari, nyumbani kwao kwa asili ambako wapo wazazi wao, wajomba zao, mabibi zao, mabinamu zao, shemeji zao, wapwaa zao, ni Zanzibar. Wakati wakionesha upendo wa pekee ambao haujawahi kutokea Duniani, kwa watanganyika, wamekosa kabisa upendo kwa ndugu zao wa damu waliopo Zanzibar. Wakaamua ndugu zao wa damu kule Zanzibar, wasinufaike kabisa na hizo neema za pekee wanazotuambia zinaambatana na ujio wa DP. Wakaamua kuziweka bandari zote za Zanzibar, nje ya mkataba. Watu hawa wana chuki kubwa sana kwa ndugu zao wa damu!!
Hawa waheshimiwa, baada ya kuhudumu kwenye serikali ya JMT, watarudi nyumbani kwao, kwa ndugu zao wa damu, waliowatenga na neema za DP!! Maana yake wameamua kuwapenda watanganyika kuliko wanavyojipenda wenyewe? Jamani ni upendo ulioje huu? Ndiyo maana wengine wamesema kuwa watu hawa wapambwe kwa maua ya dhahabu.
Jibu lisipokuwa la ndiyo, basi itamaanisha watu hawa wanawachukia mno Watanganyika, kiasi cha kuamua kuwaletea watanganyi chatu awameze, wakati kwa upendo mkubwa na wa upendeleo, wakiwalinda jamaa zao wa damu kwa kuwaweka mbali na chatu, ili hata siku wakirudi nyumbani, wawaambie ndugu zao, "angalieni ndugu zetu tulivyowalinda, hata tukawaweka mbali na gharika ili msiangamie. Tumewaokoa, tumedhihirisha ni namna gani chura ana uwezo wa kumwua tembo. Tuwadogo, tuwachache, lakini tumemwangamiza mkubwa, tumewatia utumwani walio wengi"
Kwa wasiojua ni kwa namna gani chura humwua tembo: Chura hukaa kwenye maji, hasa madimbwi na mabwawa. Tembo kwa sababu mkonga wake ni mkubwa, anapoenda kunywa maji huvuta vitu vyote vidogo vidogo vilivyopo karibu na pale anapokunywa maji, chura ni miongoni mwa viumbe ambao huvutwa. Akiingia kwenye mkonga wa tembo hujibanza ukutani, na hivyo haendi pamoja na maji kwenye tumbo la tembo. Chura asili yake ni kupiga kelele. Baada ya muda chura huanza kupiga kelele akiwa ndani ya mkonga wa tembo. Tembo kwa hasira, huanza kubamiza mkonga wake kwenye miti na mawe kwa lengo la kumwua chura, lakini kinachochakaa ni mkonga wake ambao ndiyo mkono wake unaompa maisha. Mwishowe tembo hupoteza maisha.
Ukubwa wa nchi siyo hoja, itategemea huyo mdogo umemweka wapi. Kama umemweka kwenye moyo, hata uwe mkubwa namna gani, atakuangamiza.