Upendo walionao WaTZ kwa Wakenya


Hehehe unalazimisha maombi kwa mipovu
Nimetoa shukrani kwa hayo maombi ya hao wadau lakini nikasema majirani zetu wanahitaji maombi zaidi yeti.
Ni kama kuacha mtu anayeishi nje kwa baridi na kumuombea aliye ndani kwenye kitanda chake

Umesahau sisi tunamuuguza mwanasiasa wenu mkuu bwana Lissu baada ya nyie kumpiga risasi 38 sasa mnapos ma mnaombea wengine ilifaa na nyie mjombee kwanza
 
Sababu zilizotolewa na waziri za kupiga marufuku ni kuokoa uchumi sio vurugu, kwa sababu maeneo mengi kwa ujumla maandamano yalikuwa ya amani na watu walitawanyika kwa amani kasoro kisumu tu, kwanini tusiamini kwamba serikali ya Kenya inaendeshwa na dikteta?
 
Tatizo kubwa linalokusumbua ni ukabila tu, kwa sababu Jubilee ni wakikuyu kwa hiyo huoni ukweli wa nchi ilipofikia, msiposhughulikia ukabila lazima mtaendelea kuchinjana tu
 

Sababu zako za kuniuliza swali la kinafiki lilikua nini kama tayari ulikua ulikua msimamo wako.
Hata Marekani kawaida maandamano yakihusisha vurugu lazima yadhibitiwe
Na sioni nini cha ajabu wewe kuhusisha uchumi, kwani nani asiyejua nchi ikiingia kwenye machafuko lazima uchumi utaharibika. Kenya iliingia kwenye machafuko 2008 uchumi wetu ukaharibika lakini cha kushangaza Tanzania ilishindwa kutufikia
 
Lengo langu ni kutaka kukuonyesha kwamba sababu alizotumia Magufuli kupiga marufuku maandamano ni za kiuchumi, yeye alidai kwamba watu wapate muda wafanye kazi, tulimwita dikteta wote sisi, iweje leo Uhuru atoe sababu hizo hizo asiwe dikteta?

Kama maelfu ya watu waliouliwa wakati wa PEV 2007, na malaki ya watu waliopoteza makazi yao hadi leo wanaishi kama wakimbizi ndani ya Kenya unaona sio muhimu, kama mamia ya watu wanaouliwa kila siku Kenya kutokana na insecurity sio muhimu, watu wanaokufa njaa huko Turkana sio muhimu, 48% Unemployment sio muhimu, high cost of living sio muhimu, mamilioni ya watu wanaoishi kwenye slums sio muhimu kwako, ila muhimu kwako ni GDP ambayo karibu yote ipo mikononi mwa watu elfu 10 Pekee lakini kwa sababu imeizidi Tanzania kwa kipengele kimoja tu muhimu umeridhika, basi bora tubaki na GDP ndogo lakini tunaishi maisha ya utu, kuliko maisha ya kinyama wanayoishi wakenya wengi
 
Acha kujificha kwenye kichaka cha karanga,ukweli ni kwamba, fujo na maandamano ya Kenya, hayahusu democracy, it is all about TRIBALISM,ndo maana maeneo yaliokaliwa na kina MUMBI FAMILY ni matulivu.TZ hatuna hayo.wakenya mnajifichia kwenye demokrasia huku nyuma ni ukabila.
 

Ila ile video was really disturbing ingelikuwa Tanzania pangechimbika ila ndugu zetu hawathamini maisha ya mtu wa chini.... Wakenya bado wanabaguana sana
 

Hivi unaelewa nini maana ya demokrasia, Uwezo wa mtu kuchagua atakacho au kuegemea upande autakao kwa vigezo vyake mwenyewe bila kulazimishwa ndio matunda ya demokrasia
Kama hao Wakenya wametumia ukabila kuchagua mlengo basi ndio hivyo, demokrasia inawapa uhuru huo. Na hata Kama maandamano ni ya watu wa kutokea Kabila moja cha msingi demokrasia yetu komavu Afrika inawapa uhuru huo na kuwalinda.

Tatizo ni pale wanahusisha vurugu ambapo ndio kitu wanafiki nyie mlikisubiri kwa hamu huku mkijifanya kutuombea amani. Kawaida vurugu zinaharibu ukuaji wa uchumi na zinaweza kutuchelewesha hadi mtufikie, hivyo inabidi wadhibitiwe mapema.

Kisumu hiyo itakua kitovu cha Afrika mashariki maana kuna bandari ya kisasa inajengwa pale na kwamba reli ya kisasa ya SGR inajengwa hadi Kisumu tutakua tumemaliza mchezo na ndio maana baadhi yenu wanafiki mlisubiri kwa hamu kuona hilo jiji limeungua.
 

Nimekuvumilia sana muda mrefu ukiongea upumbavu wako huo. demokrasia gani ambayo wanyonge wanauawa makusudi. mtu anakuja na kuwagonga watu bila hata kuwa na chembe ya huruma. sasa nikwambie Kenya hamna cha demokrasia wala nini ni ukabila tu umewajaa. wengi wamejawa na hasira kuwaelekea nyie wakikuyu. kuna a very serious class struggle pia kuna very serious political polarisation. kuna watu wana machungu na ukabaila na unyonyaji muliowafanyia tangu zama hizo (historical injustice).
halafu wewe unakuja hapa na ngonjela za demokrasia. demokrasia gani haijali wanyonge. mnaona mambo yako sawa tu kwa sababu mnafurahia maisha na mali ambazo mmezipata kwa kunyonya wengine. mnakula bata kwa hasara ya wengine. hilo halita waacha salama.
 
Kama hiyo ndiyo demokrasia, sasa tuambie nini maana ya tribalism?, kwa nini wajaluo walipanga kuvamia nyumba ya PLO kwa sababu tu ni mjaluo ameiwakilisha Jubilee?, kwanini yule mwanamziki wa kijaluo aliyeimba nyimbo ya kumpigia kampeni Uhuru Kenyatta alivamiwa na kukimbilia Mwanza kujificha hadi leo kwa sababu tu alisaliti kabila lake?, wakikuyu kadhaa waliosaliti jubilee walifanyiwa tambiko la kijadi na wakikuyu kuwatenga?

Zaidi ya ukabila Kenya, hakuna demokrasia yoyote japo unataka kulazimisha vitu, kukataza maandamano yaliyoruhusiwa kikatiba kwa sababu za janja janja kama alizotoa Magufuli, na hizi zilizotolewa na Uhuru kupitia Matiang'i ni ukiukwaji wa demokrasia na usijaribu kubadili nyeusi kuwa njano.
 

Pole sana kaka kwa kunivumila, lakini ndio hivyo maana hamna namna inabidi humu niwe nawapa ukweli japo mnaumia kila siku. Rais wenu husema msema kweli ni rafiki wa Mungu.
Itawachukua muda mrefu nyie kufikia demokrasia level ya Kenya, ilitugharimu sana sisi.
 
Una elements za udikteta kabisa, kwa nini muda uwe extended? Vipi kama kuna rais mbaya na katili mkae nae miaka 10 kisa ku save pesa? Hufai kabisa
 
Wewe ni muongo mkubwa,wazungu wanatofautiana utamaduni kulingana na nchi ,walivyo Wajerumani sivyo walivyo warusi, ni wazungu wa nchi gani ambao mtoto anamfokea baba? Watu tumeishi nchi nyingi sana uzunguni, acha uongo wewe, nenda Lumumba kawadanganye mazezeta.
 

hakuna demokrasia Kenya zaidi ya philosophy yenu "kila mtu akate nyama kulingana na ukali wa lisu chake" inayopalilia ukabila na class struggle.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…