Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Mada inajieleza, hayo maneno yalisikika yakitoka kinywani mwa mtu mwenye dhamana ya kutupa moto mara moja, nimejiuliza maswali;
ongezeni maswali mengine
- Wakati wa ujenzi wa hizo line, wahandisi, designers wa hizo power lines hawakujua kuwa kuna upepo hivyo wazingatie spacing ya waya?
- Miaka yote upepo umekuwa ukivuma na waya hazigongani na kama zilikuwa zinagongana je hapakuwepo namna ya kuondoa hilo tatizo? Hao wataalamu wanafanya kazi gani?
- Je ni Tanzania peke ilipotumika teknolojia iliyopo hapo Ubungo zinapogongana waya na kusababisha umeme ukatike?
- Ina maana wataalamu walipoweka hizo waya hawakujua kuwa zipo uchi wachukue tahadhari ili kuziepusha na migongano wanayoitaja
- Huo upepo mkali unaosababisha huo usumbufu umekuja na kiongozi kama yule mwingine alivyotuletea solar eclipse kule Rujewa Meya na Wanging'ombe Njombe?
ongezeni maswali mengine