Tuna mambo ya kujifunza kwa yanayotokea duniani kwa namna nyingi. King Muswati, wa Eswatini, amekimbia nchi baada ya kuona nguvu ya wanaodai demokrasia imeongezeka. Lakini tukumbuke, Waswatzi, wamekuwa chini ya uongozi wa kitemi, unaompa mtemi wao nguvu kubwa isiyohojiwa kwa mila na mapokeo yanaolindwa na imani za mizimu. Ukuta huo uliambatana na masuala kadhaa yanayovunja haki za binadamu, kama kukosa elimu sahihi y akuwasaidia katika ulimwengu huu wa utandawazi, wanawake kufanyika mashine za ngono, n.k. Somo ninalolipata mimi ni kwamba:-
1) Cheo ni dhamana. Ni vizuri kutenda mema na haki kwa cheo chako kwa maslahi mazuri ya waliokupa hiyo nafasi, pasipo hila wala ubaguzi. Watu wana haki sawa.
2) Kuna faida katika kuendeleza binadamu unaowaongoza ki elimu na maarifa ili upate watu sahihi wa kukusaidia kusimamia na kuendesha nchi. Wakiwa na elimu sahihi watapanga na kuchagua mwelekeo kwa umakini, na hawatadanganyika na mtaheshimiana. Maana ni afadhali uondoke madarakani kwa maamuzi ya kitaalam ya unaowaongoza, kuliko vurugu za watu wajinga.
3. Ujinga ni mtaji wa muda tu, mwisho wake utalemewa na hutapata wasaidizi.
4. Ngonjera na sifa kutoka kwa watu wasioelewa, ni kujilisha na upepo kwa sababu wanaweza kuimba ngonjera vile vile kinyume chako bila kutumia akili pale upepo ukigeuka.
5. Tujifunze sote, viongozi na waongozwaji kumaliza mambo yetu kwa amani na majadiliano na si ubabe wala vurugu. Na hili tu litwezekana kama serikali zetu zitapunguza kutumia ujinga wa watu kama kinga dhidi ya kukosolewa kitaalam.
6. Kujimilikisha raslimali za taifa na kuwaacha wanachi wajinga, maskini bila fursa za uchumi, ni bomu.
Ongeza na yak kwako ili tupeane maarifa.