Upepo wa tukio la Mwamposa kwa jicho la tatu

Upepo wa tukio la Mwamposa kwa jicho la tatu

obseva

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2009
Posts
574
Reaction score
648
Kumekuwepo na malumbano ya kihoja juu ya hali inayoendelea sasa kwenye mitandao ya kijamii, kufuatia tukio la Vifo vya watu kadhaa kwenye mkutano ya mtumishi Mwamposa. Jamii imegawanyika kwenye fikra mbili, ya kwanza ikiwa ni uwepo wa ujanja ujanja kwenye huduma za kiroho na wengine wakiliona kama tukio la bahati mbaya na kwamba lilisababishwa na uzembe wa uratibu wa tukio la kukanyaga mafuta.

Kilichonisukuma kuandika bandiko hilo, ni hofu ambayo imewakumba wakristo wachanga na wakati juu ya imani yao kwa MUNGU wao na haki yakukutanika kwa maana yakumwabudu MUNGU. Naiona hatari mbele kwamba Mioyo ya watu wengi inaweza kupoa na kufikri hakuna MUNGU wa kweli na pia hakuna watumishi wa Mungu wa kweli na hivyo kuamau kufuata mawazo yao na njia zao wenyewe jambo ambalo ni hatari Zaidi.

Sitaki kujadili juu ya tukio la Moshi, lakini natamani watu tuone madhara ya tukio kwa jamii ya watu wanaomwamini MUNGU na wale wanaotamani kumtegemea MUNGU, Mpaka sasa kuna watu wamekataa tama juu ya watumishi hawana imani nao, lakini neno la Mungu linatutaka tuwaamini ili tufanikiwe (2 Nyakati 20.20), kwa maana nyingine bilakuwaamini hakuna mafanikio ya KIMUNGU. Kawaida ya Moyo ukiona tukio baya hurudi nyuma, ni hatari zaidi kama mtu binafsi hawezi kuchukua hataua ya kupambanua mambo na kujaribu kuilinda nafsi yake ili asibebwe na upepo wa matukio.

Lakini tukumbuke kuwa MUNGU na Shetani wanatumia wanadamu kama watumishi wao,
hivyo si ajabu mtu kuwa agenti wa MUNGU au shetani, na kwa vyovyote vile kutumika kwa mwanadamu upande wa mema au mabaya hakubadilisha makusudi ya MUNGU juu ya wanaadamu.

Hoja za matumizi ya vitu katika uponyaji sio jambo geni hata biblia inaushahidi wakutosha. Yesu alitumia tope(yohana 9:6), Yesu aliponya kwa vitambaa, Mafuta, Yesu aliponya kwa mate, Elisha aponya maji kwa chumvi nk.(2Wafalme 2:19-25).

Hivyo sio hoja Mungu kutumia chochote kuponya, Lakini pia shetani aliweza kutumia vitu hivyokufanya maajabu, kwa mkutadhaa huo media yoyote yaweza kutumiwa either na MUNGU au Shetani cha msingi ni kujua roho iliyoko nyuma ya mtenda muujiza.

Hivyo ni vyema waamini wakawekeza kwenye kujua ukweli huo ambao Mungu ametuagiza (Wapenzi wangu, msimsadiki kila mtu asemaye kwamba ana Roho wa Mungu, bali chunguzeni kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa Mungu au la, maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguni 1 yohana 4.1)

Pia waamini wafahamu, hii ni vita ya kumiliki ufalme kwahiyo, MUNGU na Shetani wanagombaniana umiliki juu ya mwanadamu na hivyo hakuna siku vita hii itaisha na kwakuwa mlengwa ni mwandamu lazima kila wakati awe makini kuhakikisha anajipanga kuzitambua hila za uharibifu ili asikamatike (2WAKORINTHO 2:11 "Hatukosi kuzijua fikra za shetani). Na kumbuka kila siku mbinu mpya zinazuka ili vita iwe tamu Zaidi.

Rai yangu kwako Mwamini, Muujiza ni muhimu ila ni chakula cha Watoto na si watu wazima kiroho na hutokea wakati wa mahitaji mazito na kukata tamaa.

Angalia miujiza yote kwenye biblia either ilitokea kama last alternative kuokoa jambo, au Mungu kujionyesha ukuu wake, Au kuongeza imani ya watu furani
, kwa hiyo kwa watu waliokomaa na kwenye mahusiano ya kawaida na MUNGU imani na neno lake ndio uponyaji na wokovu wetu.

Jenga uhusiona usioteteleka na MUNGU kila wakati lolote linalopita kwako litaondoka lenyewe. Kama kuna tukio linalotka kwa MUNGU kwa ajili ya rekebisha kitu utaopata ufunuo juu ya tatizo lako maana Mungu hapendi mwanadamu ateseke.(kumbukuka mwiba ya Paulo, Neema yangu yakutosha).
 
Hawa wanaojiita mitume na manabii, na wafalme, Kuna siri kubwa nyuma ya pazia

Huyu ndie yuko nyuma ya huduma zao anaewawezesha kufanya ishara na miujiza anaitwa;

NANA KWAKU BONSAM
20200206_122022.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie mnaojifanya kuja kuneutralize mambo ndio mnawapa kichwa hawa matapeli na kuzidi kuwapoteza watu. Biblia imesema nimekupa bure toa bure. (Mathayo 10:8) Jambo la msingi la kujiuliza mafuta au maji yaliyotumika kwenye Biblia yaliwahi uuzwa au kutolewa kibiashara? Jibu ni HAPANA. Sasa je kibali na mamlaka ya kuuza haya maji wanakitoa wapi? Wanatumia andiko lipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie mnaojifanya kuja kuneutralize mambo ndio mnawapa kichwa hawa matapeli na kuzidi kuwapoteza watu. Biblia imesema nimekupa bure toa bure. (Mathayo 10:8) Jambo la msingi la kujiuliza mafuta au maji yaliyotumika kwenye Biblia yaliwahi uuzwa au kutolewa kibiashara? Jibu ni HAPANA. Sasa je kibali na mamlaka ya kuuza haya maji wanakitoa wapi? Wanatumia andiko lipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa ndio wanawapa kichwa hawa matapeli


Tujiulize maswali machache



HAYA TWENDE KAZI

1. Alete mandiko wapi Yesu au mitume au manabii waliuza mafuta ,maji ,keki ,chumvi kwa mgongo yana upako

2. Kwanini hayo mafuta ya upako , kama yanaponya ,hayajawaponya majeruhi kule moshi, zaid Yule Tapeli alikimbilia dar kuwahi hela za misukule wengine

3.Ametoa maandiko kuhusu mafuta kutoka ,lkn hatuoni yakiuzwa


4.Inakuwaje hawa matapeli wanaojiita manabii kila mmoja ana kanisa lake , na mafundisho yake tofaut na wenzake , lkn Wanadai wametumwa Na Mungu?

AJIBU HAYO MASWALI
 
Back
Top Bottom