Upi bora kati ya hii mikopo ushauri wenu

janjab

Senior Member
Joined
May 28, 2015
Posts
172
Reaction score
56
Nina mkopo wa nmb ambao umebaki kiasi cha tzs 2,031,474.10 ambapo niliamua kwenda crdb kuona kama wanaweza kununua deni hivyo nilifika na afisa mikopo alinipigia hesabu akanambia naweza kupata tzs 9,500,000 ambapo akanipa barua ya kuomba balance ili mkopo wangu nikipewa kiasi cha pesa kingine kitumike kulipa mkopo, nmb pia makato akanambia yatakuwa 231000 kila mwezi,alinambia pia kuna makato ya bima na ya proces za mkopo bima alinambia 118000 nilipa hesab nikaona napata kama m.7 na laki kadhaa baada ya makato yote..........baada ya hapo nilienda nmb kuona nao wananambiaje nilipofika afisa mikopo alipiga hesabu akanambia kuwa naweza kupata 11,300,000 toa deni langu ambalo ni 2,031,474.10 na bima +fedha ya kuprocess mkopo ambayo ni kama 769548.14 wakanambia naweza kupata net tzs 8.498.977.76 baada ya makato yote na makato kwa mwez ni 245,117.80 na nalipa kwa miaka sita.swali langu ni je? Kwa mchanganuo huo hapo juu ni bank gani naweza kuchukua mkopo kati ya hizo hapo juu kat ya nmb na crdb
 
CRDB wao walinambia muda ni 5 years
 
Unakopa mkopo wa muda mrefu sana hata kukushauri nashindwa
 
Usipende kuchukua mkopo wa muda mrefu hivyo. Jitahidi kuchukua mkopo mwisho uwe ni miaka mitatu tu.
 
Usipende kuchukua mkopo wa muda mrefu hivyo. Jitahidi kuchukua mkopo mwisho uwe ni miaka mitatu tu.
Kuna wakat inabidi mana mf mm bodi heslb wamekula sasa ukichukua ya muda mfup means makato yanaongezeka na unajikuta sheria ya 1/3 inakufyekeleaa mbaliii
 
Kwa hesabu hizo hapo mkuu CRDB is ze best,na ukichukua kwa,miaka sita huko crdb utachukua mkwanja mrefu zaidi
 
Mkopo wa mwaka mmoja ni mzuri sana kwasababu kama kuna sehemu (biashara) mekosea nirahisi kurekebisha
 
Mkuu CRDB na NMB makato yao ni sawa tofauti ni unatyaka miaka mingapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…