beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Mbunge wa Jimbo la Makete, Mhe Festo Sanga amehoji Bungeni leo kuhusu Soko la Parachichi.
Namnukuu:
"Soko la Parachichi Duniani linasomeka parachichi zinazalishwa Nchi jirani ya Kenya, ili hali Parachichi asilimia zaidi ya 50 zinazotoka Ukanda huu wa Africa Mashariki zinatoka Tanzania, Wanunuzi wanazibrand kama zinatoka nchi jirani na sio Tanzania.
Upi Mkakati wa Tanzania kutengeneza-Ownership (Umiliki) wa Soko la Parachichi kwa kuanza kuzibrand kama product ya Tanzania"?. Mwisho wa kunukuu.
Majibu ya Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe, yameonesha kuna mpango wa Serikali kuanzisha common use facilities kwa ajili ya kuanza kuziprocess parachichi na kuziandika kuwa zinatokea Tanzania.
Lakini, amekiri kuwa ni kweli parachichi zimekuwa zikinunuliwa kama raw materials na kwenda kuandaliwa vizuri huko nje kisha kuwa branded na nchi husika.
My Take: Tulichelewa sana kwenye hili. Mbunge Sanga amefanya vizuri kulipambania. Tuhamie na kwenye mazao mengine pia.