Upi mtazamo wako juu ya kipindi maarufu cha Jahazi kufungiwa?

Jamaa kauliza mitazamo ya watu. Watu wakitoa mitazamo anaipinga.
 
Kuna vipindi havihitaji kuwa seriously na kukaza uso ili kukiendesha.
Ni soga tu Kama kijiweni na kipindi kinaenda swaafi kabisa.

La muhimu kusiwe na maneno mengi yenye ukakasi Kama aliyokuwa anayatoa Marehemu Kibonde..yule alikuwa mropokaji haswa

Radio nyingi na hata vituo vya TV hapa nchini vipindi ni hovyo tu, wanaita ni radio za burudani lakini hata burudani ina uwasilishaji wake basi!
 
Kipindi Changu Safi Cha wakubwa ni MAZUNGUMUZO YA FAMILIA pale redio one siku ya jumapili. Hakina matangazo na unajifunza na kuburudika. Hawa wwngine acha wafungiwe tu.
 
Pole yao..ila wamestahili.
 
Hii kasumba ya kuokoteza watu waropokaji wasio na weledi na kuwapa vipindi haina afya kwa tasnia ya habari, eti wanaojiita ‘wachekeshaji’ ndo wamekuwa watangazaji!!
Hakuna watangazaji hapa, hakuna wahariri na hakuna waongozaji. Ni vikundi vya wahuni vinavyokutana kupiga soga kwenye vipaza sauti. Periodt

Kila kipindi wanakuja kufreestyle tu. Ukiwauliza wanataka kuachieve Nini mwisho wa kipindi chao.. hakuna anayejua.

What are the news bits, ili tuwapime mwisho wa kipindi? Kama walifanikiwa... hakuna ajuaye.. Ni patashika nguo kuchanika na sio uwadhaniao. Wanapopita ukiwauliza... Hakuna ajuaye..

Na ukiitisha kila redio Leo hii...waje na work plan ..utashangaa ..vichwani empty empty tupu. Yaani wanaongozwa na hype..

Wakishangiliwa wanashikiria humo humo. Kwa wanahabari huo ni uzwazwa lazima uwe controller of the narrative..sio unazurula tu Kama kucheza kiliwanzenza.

Mwana habari wewe Ni mwalimu wa Umma. Sasa unaachaje wanafunzi(Umma) wakuendeshe kisa unasifiwa.. unakuwa punguani. Unaropoka kila ujinga bila kujua hadhira yako ni mchanganyiko kwa muda ulioko hewani.

Kwenye daladala watoto wanatoka mashuleni wapo wazee, walimu wao na kila Aina ya watu...mtu Mzima upo redioni umekazana na pungeto..[emoji16][emoji16][emoji1241][emoji119]

Hawa watu wanahitaji bodi. Wakitoka shule wakakae Kwanza kwenye kukusanya taarifa na kuhariri mpaka waive ndio wapewe nafasi ya kukaa nyuma ya vipaza sauti. Na huko wakizingua leseni inafutwa na akae miaka minne akijifunza ndio arudi tena kwa kusoma ripoti za mikoani.

Upuuzii hatutaki.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Leo nimesikia wamefungiwa wiki mojahiyo radio kwa kutangaza habari za wagombea ubunge kupita bila kupingwa bila ya kuwa na uthibitisho.
 
Leo nimesikia wamefungiwa wiki mojahiyo radio kwa kutangaza habari za wagombea ubunge kupita bila kupingwa bila ya kuwa na uthibitisho.
Ina maana hawakuongea na Nec ili kupata uhakika?
 
CLOUDS FM/TV NI WATOVU WAKUBWA WA NIDHAMU
ADHABU IONGEZWE pia watu wao hawana taaluma yeyote ya uandishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…