Upi ni ukweli kuhusu bara la Atlantis

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
20,537
Reaction score
31,729
Kama title inavyosema kwa wajuvi wa mambo humu JF je upi ni ukweli kuhusu historia kwamba kulikuwa na bara linaitwa atlantis lililoongelewa na mwanafalsafa wa kigiriki Plato kwamba lilikuwa na teknolojia kubwa kuliko hata ya sasa ila lilipotea kutoka uso wa dunia maana ilidaiwa lilikuwepo kati ya bara la ulaya na amerika kaskazini je ni kweli hili bara lilikuwepo ??? Na kma lilikuwepo limeenda wapi???

Ahsanteni

BAADHI YA MAJIBU
 
Bara la Atlantis kipindi cha Nuhu kurudi nyuma lilikua likitumiwa kama Base/makazi ya Viumbe waliopatikana baada ya Fallen angels kuingiliana kingono na binaadam (WANEFILI)
Baadae lilipotea hilo bara na kubaki barafu tu lakini mpango uliopo sasa hv under secret societies (Iluminat) ni kulirudisha tena na kurudisha Nephilism bloodline. Soon we are reached NWO
 
...Samahani mkuu naomba kueleweshwa kidogo hivi Fallen Angel walipokutana kingono na Binadam Ndipo akazaliwa Nephilims!??au Nephilims walikuwepo kabla ya Fallen Angels.??ni hayo tu ntashukuru
 
Fallen angels..wakiongozwa na Azazel ndio waliingiana na binaadam wakatokea Nephills so Nephils ndo Product ya Fallen angel.

Remember baada ya hao malaika 200 kushuka duniani Mungu aliwafunga kuzimu Wakisubiri hukumu yao ila Nephills bliidline waliondolewa na Gharika kuu ya Nuhu..

...Samahani mkuu naomba kueleweshwa kidogo hivi Fallen Angel walipokutana kingono na Binadam Ndipo akazaliwa Nephilims!??au Nephilims walikuwepo kabla ya Fallen Angels.??ni hayo tu ntashukuru
 
...Samahani mkuu naomba kueleweshwa kidogo hivi Fallen Angel walipokutana kingono na Binadam Ndipo akazaliwa Nephilims!??au Nephilims walikuwepo kabla ya Fallen Angels.??ni hayo tu ntashukuru
Nephillism hawakuwepo before walikuja kujitokeza baada ya falling angel kuwa sex binadamu ,na hali haikundulika mapema ilikuja onekana baada ya mitoto kuwa mikubwa bila kikomo ndo wakashamga nakuanza kujiuliza what happen
 
Nikajua majibu unayo
Nimesoma article mbalimbali na hicho kitabu cha criteas cha Plato amegusia habari ya atlantis kuwa ni bara liliozaa maendeleo yote tunayoyaona leo ila lilizama baharini sasa theory nyingine inadai ndio Antarctica ya sasa ndio maana nkaona nilete humu ili nipate feedback nzuri zaidi kwa waliopitia nadharia hii

Ahsante
 
Ok kama waliondolewa na gharika ya Nuhu kivp wana wa israel walipotaka kuingia Cannan waliogopa sababu walikutana na majitu makubwa hadi wao kuonekana kma panzi tu........ Je hao majitu makubwa kma wanefili walitokea wapi ilihali gharika lilikwisha???

Je kizazi cha Aruba na Annunaki vilitokea wapi
 
Mkuu
Kama sijakosea.Baada ya Gharika Mungu aliziacha nafsi za hao wanefili hai ili vizazi vyote vije vishuhudie yaliyotokea..

Lakini hizi nafsi pia ndio zilianza tena kazi kuendeleza ubaya kwa kuwatumia watu..
Ndio zilizomwongoza nimrod kujenga Mnara wa babeli..
Pia zinafanya mengi makubwa kwa kupitia binaadam wenyewe eg Illuminat.

Suala la kanani naweza sema kua hao hawakua wanefili bali tu itakua ilikua tu kutokana na asili ya majimbile ya watu mfano Muha wa mkongoro akisimama na msukuma wa shinyanga lazima ajione panzi maana kiasili waha wafupi wasukuma warefu.

Pia mfano Goliath alikua ni jitu kubwa lenye mwili uliopanda juu lkn si Wanefili.

So suala la hapo kanani si dhani kua walikua wamewaona wanefili.

Hao uliotaja paragraph ya mwisho siwafaham labda unielezee nipate elimu
 
Nakumbuka nilipokuwa Mwenge Sec (Singida) mwaka 1972 nilipendelea sana kusoma vitabu vya Erich von Däniken. Huyu mwandishi ameandika vitabu kadhaa vinavyohusu Atlantis. Kitabu nilichokirudia rudia na hadi sasa nakikumbuka ni Chariots of the Gods? na vitabu vingine. Ni muda mrefu sana umepita na hiyo ilikuwa shauku ya ujanani ingawa kwa sasa siamini tena haya masuala. Tafuta vitabu vya huyu Erich von Däniken ameeleza sana kuhusu "extraterrestials" ambao waliitembelea dunia zama za kale. Na nadhani kwa zama hizi za utandawazi inawezekana kuna video zake youtube pia; kwa sababu ameshatengeneza DVDs na vipindi (documentaries) kadhaa vya television.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…