hapa kuna maswali mengi na wengi wetu wanayajua lakini kwa vile waliounda muungano huu walikuwa na interests zao zingine ambazo either zimepitwa na wakati au wanajua kuwa unaficha udhaifu wa walio wengi.
Binafsi nadhani Kisiwa cha Pemba, Zanzibar, Mafia nk wakazi wake wengi wako na uhusiano wa moja kwa moja na upande wa bara. Aliyevitenganisha ni hao wageni ambao walikuja kufanya shughuli zao na wakaamua kulowea. Nimeangalia Channel 10 juzi wakielezea historia ya Kilwa Kisiwani jinsi kilivyowahi kununuliwa na mfanyabiashara mmoja wa Kishiraz karne ya 7-9 kwa kipande cha nguo, lakini leo hakina mgogoro wa umiliki. Ni sehemu ya Tanzania!
Ukiangalia vizuri historia ya Zanzibar ukiihusisha na Tanganyika inaleta jambo jipya (wengi tunalijua) ambalo ni Kilomita 10 za mwambao (kutokea mwambao wa Mombasa mpaka sehemu za Msumbiji) ambazo tukiendelea na mawazo tuliyonayo sasa huenda zikaanza 'kudaiwa' nazo! Pia kuna baadhi wanaodai kuwa Pemba haikuwahi kuungana na Unguja!
Kwa ujumla ukianza kuongelea haya mambo utasikia wengine wanasema mara "oh, wewe haya mambo ya Muungano huyajui, ...oh! hujui historia" nk. Yaani haina tofauti na 'siasa (uswahili) za simba na yanga'!!
Lakini matokeo ya haya yote ni kuwa nchi hii (ikijumlisha pande zote mbili) pamoja na kuwa na utitiri wa rasilimali zimekosa kuendelea kwa aidha kuchelewesha maamuzi au kwa kutokuwa na maamuzi kabisa sabau ya 'MUUNGANO'!