Upi uhalisia wa Takwimu za sensa kwamba Wanaume ni 50% na wanawake ni 50%?

Upi uhalisia wa Takwimu za sensa kwamba Wanaume ni 50% na wanawake ni 50%?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

Takwimu za sensa iliyofanyika mwaka 2022 inasema Tanzania yetu wanaume na wanawake idadi Yao ni sawa Kwa asilimia, ingawa katika namba, inaonyesha wanawake wamewazidi wanaume Kwa 46,000.

Takwimu za mwaka 2022 zinasema jumla kuu ya population ni 67,760,837.

Wanaume- 33,857,364.(50%).

Wanawake-33,903,474.(50%).

Hapa tunavyoongea, July 2024 Kuna ongezeko la watu zaidi ya 1,700,000. Maana population ya sasa inasoma 69,428,058.

Swali; Unauongeleaje uhalisia wa Takwimu hizi kuwa idadi ya wanawake na wanaume ni sawa, kwamba katika familia Yako, ukoo au JAMII uliyopo, idadi wanaume ni sawa na wanawake?

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni🙏
 
Vijana hamtaki kuoa ndiyo maana inaonekana kama vile wanawake ni wengi kuliko wanaume.

Kila kijana angeoa uhalisia wa data hizo za sensa ungeonekana (japo sina uhakika kama data hizo ni sahihi!)

Nahisi kama vile niko nje ya mada. Mi K-Vant hii nayo ni kero tupu 🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️

Screenshot_20230822_151355_Instagram Lite.jpg
 
Mkuu hizo takwimu hazina uhalisia wowote, nafikiri kwa miaka ya hivi karibuni kuanzia 2000 na kuendelea takwimu sahihi za ke na me unaweza kuzipata kwa usahihi kwa msajili wa vizazi
 
Hii nchi ukiambiwa Jambo usiliamini moja kwa moja kila mtu ni muongo muongo, kuanzia serikali mpaka watu wake.
Sisi ni waongo, wajanja wajanja.
 
Mkuu hizo takwimu hazina uhalisia wowote, nafikiri kwa miaka ya hivi karibuni kuanzia 2000 na kuendelea takwimu sahihi za ke na me unaweza kuzipata kwa usahihi kwa msajili wa vizazi
Ukienda mahospitalini, mwanamke akizaa mtoto wa kiume anapongezwa, unakuta siku nzima, kati ya watoto waliozaliwa kituo Cha AFYA kama ni kumi, wanaume ni wawili au watatu, waliobaki ni wanawake.

Hiyo 50/50 imetoka wapi?
 
Wanaume- 33,857,364.(50%).

Wanawake-33,903,474.(50%).

Takwimu zimepikwa, ni sawa na wale watu wa kijiweni wanaosema kuwa dini mbili za kigeni za kuja kwa bahari Tanganyika kwa majahazi na merikebu ni asilimia 50 / 50 .

Kisayansi idadi ya wanaume na wanawake haiwezekani kuwa 50/50 asilimia.

Wanaume wanachangamoto kibao ambazo zinazuia idadi kukaribiana 50 / 50 asilimia baina ya wanaume na wanawake ktk idadi jumla ya watu.

USA 🇺🇸:
Projection estimates calculated using the mid-term population ration of 49.5 percent male and 50.47 percent female - constant with US Census data for 2021. 2010-2021 values calculated based on the US Census population characteristics for 2010-2019 and 2020-2021.
 
Cooked data.
 
Back
Top Bottom