Upi wakati sahihi wa kubadili GearBox Oil (ATF )

Upi wakati sahihi wa kubadili GearBox Oil (ATF )

IST recommended ni Type IV inauzwa Elfu 90 Lita 4 zinaingia itabaki kidogo.

ATF ni life time according to manual. Pia ukitoa stick ya ATF utaona wameandika no need to change under normal driving conditions.

Ila kama una hela nunua tu badirisha. You will notice some changes.
 
Siku ukikosea ukabadili ATF basi unaipoteza gearbox hapohapo.Msingi wako inatakiwa uwe ni manual ya gari yako na wala siyo porojo za watu wa JF au mimi.

Utajitetea kuwa huna manual ila manual za IST zimejaa google kuliko wabunge fake wa CCM walivyojaa bungeni.Hii maana yake ni kwamba wewe kuwa dilemma ni suala la kujitakia wewe mwenyewe.Nimekuonyesha njia,chukua hatua sasa!
 
sikushauri kubadiri gearbox oil kama hmna shida yeyote umepata ktk transmittion maana ukicheza vibaya na io service jiandae kisaikolojia though waweza fanya as proper maintenance ya gari aftr 9000km au kila baada ya service ya engine x3

na shida hasa huwa inaanzia pale unapotoa gear box oil yenywe na kuweka mikorogo cz lazma gear box oil number ziwe sawa unapotoa ndo io io irudishwe
 
Yaani mtu unashaurije mwenzio asibadirishe ATF?
Wao wenyewe (Toyota) wameandika kwamba hakuna haja ya kubadili ATF kwa matumizi ya kawaida ya gari. Shida ni kwamba sisi hatutumii ATF quality kama wanazoweka kiwandani, zinazoweza kukaa hadi 200,000/= km. Hizi tunazoweka sisi, kagua tu kuona kama imekuwa nyeusi, ukiona imekuwa nyeusi sana, badilisha.
 
Unaposema hatutumii quality kama za kiwandani unamaanisha nini? Maana Toyota wenyewe wanayo ya kwaio na inauzwa dukani kwao Toyota...au unamaanisha zile za 7,000 1Litre
 
IST recommended ni Type IV inauzwa Elfu 90 Lita 4 zinaingia itabaki kidogo.

ATF ni life time according to manual. Pia ukitoa stick ya ATF utaona wameandika no need to change under normal driving conditions.

Ila kama una hela nunua tu badirisha. You will notice some changes.
IST unawaza kubadili ATF ili ugundue nn? IST hata ikiungua mi naona sawa tu
 
Shida ni kwamba, unakuta owner wa kwanza alishabadirisha na akaweka zile cheap ATF.
Magari yenyewe ya kibongo haya gear box tunanunua laki 3 hadi 4 pale Shauri moyo, sioni hata haja ya kujipa pressure sana, weka tu ATF ya kawaida, 7k per liter, tembelea kilomita elfu 10 kisha kagua kama ule wekundu umeondoka na kuwa nyeusi, kama ni nyeusi means imeshaungua, badili
 
Gearbox ya IST zinauzwa 1.8 million hapa Gerezani Kariakoo
 
Back
Top Bottom