Kwa wale tulizoea upigaji kura katika enzi ya vyama vingi, tofauti na wakati wa Mwl. Nyerere ambapo kulikuwa na kupiga kura ya ndiyo na hapana kwa ngazi ya urais, ni jambo la kawaida kuwa kila mgombea wa chama humweka wakala wa kusimamia kura zake hasa wakati wa kuhesabu. Baada ya kura zote kuhesebiwa na kujumlishwa wakala pamoja na mgombea husaini fomu ya matokeo katika ngazi husika. jambo kubwa linalohakikshwa hapo ni kuwa kila mgombea anatendewa haki na kwamba kura zake hazichakachuliwe kwa mfano kupewa mgombea mwingine.
Katika upigaji wa kura za maoni kutakuwa na pande mbili zitakazokuwepo, yaani watakaopiga kura ya "hapana" na watakaopiga kura ya "ndiyo". Kwa hakika kila upande utapenda kuamini kuwa msimamizi atende haki kwa kuheshimu maamuzi ya kila mpiga kura. kati enzi yetu hii ambayo tume yenyewe ya uchaguzi haiaminiki, ni utaratibu upi wa kuhakikisha kuwa kura ya kila mtu itakuwa salama? Je, kutakuwa na utaratibu wa kuwepo mawakala, na mwakala halali watapatikanaje?