Nani asiyezijua mashine za EFD au hizi zinazotumiwa na jamaa wa parking au kwenye malipo mbalimbali?
Mashine hizi sasa ni takwa la kisheria kwa wafanya biashara vinginevyo hakuna kufanya biashara.
Uliza bei za hizo mashine. Si ajabu kusikia 600,000/- kwa moja na malipo lukuki ya mwezi kwa matumizi.
Kwamba serikali inakopeshwa mashine hizi kwa bei inflated na wananchi hawa ambao ni maskini mno wenye kusongwa na mizigo ya tozo? Kwamba kumbe eti mashine hizi ni mali ya serikali?
Kwanini serikali isizinunue yenyewe mashine hizi na kuwagawia watu badala ya kuwalazimisha kuikopesha?
Kwanini mashine hizi kama ni muhimu kwa serikali zilipiwe na serikali kwa bei ambazo ni za kitapeli?
Kwanini kama zi muhimu kiasi hicho serikali isizilete mashine hizo kwa bei zake halisi kutokea China huko?
Tutaendelea kupigwa na kunyonywa kiujanja ujanja hivi na walamba asali hadi lini?
Mnapotakiwa kuachia ngazi tambueni mna makando kando mengi. Wachawi ni nyie wenyewe.