Upigaji mpya wa fedha za wazazi jijini Arusha Kamati za Wazazi Shule za Serikali

Upigaji mpya wa fedha za wazazi jijini Arusha Kamati za Wazazi Shule za Serikali

Sir luta

Senior Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
163
Reaction score
221
Salam wanabodi,

Upigaji wa fedha za wazazi ni upigaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa kamati za wazazi katika shule za serikali hasa za sekondari. Karibia kila shule wazazi wamefungua account bank kwa ajili ya michango ya chakula cha watoto shuleni, mpishi, walinzi, walimu wa masomo ya sayansi, kwa makubaliano yao. Wakachagua kamati yenye Mwenyekiti, Katibu, Mweka Hazina na Mjumbe mmoja na wote wanakuwa watia saini benki katika hiyo account na ndio wenye mamlaka ya kutoa pesa kwenye hizo account kwa ajili ya malipo.

Sijui Sheria za fedha za umma zinasemaje lakini hizi account hazikaguliwi. Siyo ukaguzi wa ndani wala wa nje; mwaka mmoja, miwili, mitatu, minne, na kuendelea hazikaguliwi na ni account zinazopokea mpaka Tsh. milioni mia moja na kuendelea kwa mwaka toka kwa wazazi lakini hakuna ukaguzi (auditing).

Tatizo linakuja watoto hupeleka bank slips shuleni kuonyesha malipo yaliyolipwa na wazazi wao kwenye account lakini wanapata huduma duni ya chakula na hakuna mwalimu wa kuwatetea maana hawahusiki na upatikanaji wa chakula hicho, hata wazazi hawawezi kuhoji chochote maana hawasomewi mapato na matumizi kwenye vikao inabaki tu "Kama unataka mwanao ale, lipa hutaki usilipe".

Lakini pia pindi wapishi, walinzi na walimu wa sayansi wanahitaji mishahara huenda kudai kwa Mkuu wa Shule maana wameingia mkataba na Shule. Kulingana na bank slips za watoto zinaonyesha pesa zipo kwenye account lakini viongozi wanasema hakuna pesa na kuanza kupiga chenga huku anayesumbuliwa ni Mkuu wa Shule na yeye Wala walimu wake siyo watia Saini kwenye account hizo.

Wapo baadhi ya viongozi wanaosimamia account hizo wamekuwa miungu watu; wanakoromea walimu, wanakoromea wazazi wenzao, hawamsikilizi mkuu wa shule, na wengine unakuta ni viongozi wa CCM. Wakati wa kuchagua viongozi hao, wao hutumia ujanja wa kuwa wasemaji na wajuaji kwenye vikao ili wachaguliwe lakini Wana mipango Yao.

Hata watoto wao wanapohitimu masomo katika shule husika, Bado huazima watoto wa watu wengine na kujidai ni watoto wao au wa ndugu zao wanawasaidia ili tu wasitoke kwenye hizo nafasi za uongozi. Uendeshaji wa hizi account umegubikwa na upigaji wa fedha za chakula Cha watoto toka kwa wazazi huku huduma zikiwa duni sababu hazikaguliwi na hata hao walimu Wanaweza wakafanya kazi miezi hata mitatu hawajalipwa lakini fedha zinaonekana zimewekwa kwenye account. Hivyo kuwepo kwa migogoro ya chini chini kwenye hizo shule.

USHAURI: Mwajiri aweke utaratibu wa kukagua hizo account kila mwaka kwa maslahi ya umma ili kuboresha huduma na kuondoa hiyo migogoro ya chini kwa chini.

Au, Baraza la Waheshimiwa Madiwani chini ya Mkurugenzi na Kamati Yao ya Fedha na Uchumi wakubaliane watafute kampuni (private entity) ya kukagua hizo account kila mwaka na taarifa ipelekwe kwenye Baraza ili wale wanaokula pesa za chakula cha watoto wachukuliwe hatua stahiki. Na hao viongozi wanaotafuta nafasi za kusimamia account hizo bora walipwe posho na hao wazazi kuliko kujifanya wanajitolea halafu wanaenda kuwa wapigaji na wezi.

Naomba kuwasilisha.
 
Pesa zinachangiwa na wazazi zina tunzwa na hao wazazi watoto niwa wa wazazi hao hao hapo tatizo liko wapi? Wewe wataka pesa zitunzwe na waalimu wenye njaa wasio kua na uchungu na watoto, hiyo ni private arrangement serikali haingilii kabisa.
 
Watu wamejifungulia account yao na wala sio ya serikali sasa hapo serikali inahusikaje hiyo ni sawa na account ya vikundi vya upatu
 
Hadi milioni mia! Hapo umeweka chumvi na magadi pamoja. Hizo kamati ni za wazazi na fedha ni zao na upo utaratibu wao , kwa hiyo km wewe ni mzazi au mlezi fuata taratibu. Huo mpango wa chakula hauko sawa kwa kila shule na hata kwa kila mkoa au wilaya kwa hiyo hata changamoto haiwezi kuwa sawa kila sehemu. Km kuna shida eneo lako wasiliana na viongozi kuanzia kijiji au mtaa ambako shule ipo.


Hadi milioni mia"
 
Pole mkuu!!! Kuna kamati moja ya shule ya serekali nikiamaka kwenda jobu namwona mjumbe wa kamati ya shule katoa kiti na meza anapambana daah, yaani kama nae ni mwajiriwa anaenda kibaruani
 
Ukitazama kwa juu juu bila kutafakari unaweza ukkahisi ni upigaji kama unavyo sema lakinj katika hali halisi tafakali mambo yafuatayo;

Mwanao anaondoka nyumbani saa kumi na mbili na nusu asubuhi kwenda shuleni ambako atakaa mpaka saa kumi na nusu jioni akisoma wakati huo hajanywa hata chai wala uji, unahisi hata huyo mwalimu anapo kwenda kumfundisha anaweza kumusikiliza na kuelewa kweli?

Pili tafakali shule ina wanafunzi elfu mbili na mia tatu hamsini na sita ila wakati huo huo walimu waliopo ni walimu 16 pekee na ina walimu wawili tu wa Basic mathematics na mwalimu mmoja wa physics na chemistry, unahisi watamdu kuwafundisha watoto hao wote kwa uchache wao? Kuna dhambi gani wazazi wakikubaliana kuchanga na kuajili walimu wa mda ili kutatua changamoto walizo nazo?

Kama fedha wanachangishana wao kwa wao na wanatumza wao wenyewe na matumizi wanafanya wao wenyewe kwa manufaa ya watoto wao wwnyewe
 
Ukitazama kwa juu juu bila kutafakari unaweza ukkahisi ni upigaji kama unavyo sema lakinj katika hali halisi tafakali mambo yafuatayo...
Soma post vizuri. Mzazi anachangia, mtoto anasoma lakini huyo mwl aliyeajiriwa na hiyo pesa aliyotoa mzazi hapati mshahara wake.
 
Huyu John Mongela ana undugu na raisa Samia? Kila kukicha ufisadi Arusha alafu hatolewi
 
Back
Top Bottom