Upigaji wa Wachina Katika Mikataba ya SGR Uko Wapi?

Upigaji wa Wachina Katika Mikataba ya SGR Uko Wapi?

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
12,096
Reaction score
15,393
Kipchumba Murkomen kafanya kweli huko Kenya.

Sasa watu wanajiuliza, ule upigaji mkubwa uliokuwa ukisemwa kuhusu unyongaji wa mikataba ya kichina upo wapi?

Bandari ya Mombasa iliyodaiwa kuwekwa rehani haionekani popote.

Na kama kuna chembechembe zozote za upigaji, ni dhahiri kabisa kwamba ni ule uliofanywa na viongozi wa Kenya wenyewe na siyo wachina.

Kuna funzo muhimu sana katika swala hili kwetu sote.
 
Documents zake nadhani ni hizi hapa. Hebu soma halafu nakuja tulijadili hili swala.
IMG_20221106_233630.jpg
IMG_20221106_233632.jpg
IMG_20221106_233634.jpg
IMG_20221106_233636.jpg
 
Ndugu, huo ni mkataba wa mkopeshaji (Exim bank of China) wa SGR na sio mkataba wa ujenzi wa SGR. Madudu kwenye mikataba yanakuaga kwenye construction contracts na sio kwenye Lender and Borrower.
 
Ndugu, huo ni mkataba wa mkopeshaji (Exim bank of China) wa SGR na sio mkataba wa ujenzi wa SGR. Madudu kwenye mikataba yanakuaga kwenye construction contracts na sio kwenye Lender and Borrower.
Bado sijakuelewa.
Una maana mkataba wa ujenzi utahitaji kuwekwa rehani bandari ya Mombasa, na hilo lisiwe takwa la mkopeshaji?

Hapa nadhani unatafuta kuchanganya tu mambo bila ya sababu zisizojulikana.

Na kama kuna hiyo mikataba mbadala ya ujenzi ambako kuna upigaji, ni dhahiri walioweka mbele upigaji huo ni viongozi wa Kenya wenyewe, na wala siyo wachina.

Kwa mfano: Bei za kufidia ardhi katika maeneo ujenzi ulipofanyika, gharama zake zipo juu sana, na kuifanya gharama yote ya ujenzi wa reli hiyo kuwa wa ghali zaidi. Wapigaji hapa ni wakenya wenyewe.
 
Documents zake nadhani ni h
Kuna walio na muda wa kusoma yote hayo, na tayari wamekwishatoa mhtasari wa mambo muhimu yaliyokuwa yakihusishwa na mkataba huo kutoonekana popote ndani ya maandishi hayo.

Kwa mfano, kuwekwa rehani kwa bandari ya Mombasa haionekani mahali popote katika mkataba wote.
 
Ndugu, huo ni mkataba wa mkopeshaji (Exim bank of China) wa SGR na sio mkataba wa ujenzi wa SGR. Madudu kwenye mikataba yanakuaga kwenye construction contracts na sio kwenye Lender and Borrower.
lakini kipengere cha bandari ya mombasa kuwekwa rehani kingeonekana humu
 
Huu uzi kwanini unajadiliwa na Watanzania , kuna nini mmekiona ?
 
Mambo ya kitaalamu kwetu wengine magumu. Anaposema preferential buyer sijui anamaabisha nini!
Hapo hakuna ugumu wowote, na wala haihusiani kabisa na kunadisha bandari, na hakuna cha "utaalam" wowote hapo.

Hilo ulilogusia ni ununuzi wa vifaa vya ujenzi na uendeshaji wa mradi wenyewe.
Ananasisitiza (hakukataza moja kwa moja), kwamba manunuzi yafanywe uchina, palipopatikana mkopo.

Hili ni sharti jepesi sana lisilokuwa na nguvu yoyote katika mkataba huo, tena unaweza kusema kwamba ni faida kwa mradi wenyewe, kwa sababu hapatakuwepo na ucheleweshaji katika kutafuta vifaa, na mnyororo wa uwasilishaji wa vifaa hivyo utakuwa unajulikana vyema.
Swala unaloweza kuhoji ni kama hayo manunuzi bei zake ni mbaya, au vifaa vinavyonunuliwa havina viwango. Hilo ni swala tofauti kabisa.
 
Huu uzi kwanini unajadiliwa na Watanzania , kuna nini mmekiona ?
Kwa sababu tulishaambiwa mara nyingi sana kwamba wachina ni hatari sana katika wizi wa mali za nchi zinazoendelea. Mikataba yao ni ya kuwanyonga nchi maskini, wakilazimisha kuweka rehani mali zao adimu ambazo huishia katika kuchukuliwa na hao wachina.

Kuna hiyo habari ya mradi wa Bandari ya Bagamoyo, mengi sana yamesemwa juu yake, lakini hata siku moja hatujawahi kuonyeshwa yaliyomo ndani yake yanayopelekea nasi sote tuimbe wimbo wa kuwakataa wachina.

Tanzania nasi tulitaka kuwapa wachina wajenge SGR yetu, unakumbuka? Tukaambiwa Magufuli alikuwa akilala na mafaili kitandani, na mwisho wa siku kagundua madudu ambayo tungeumizwa nayo juu ya kazi hiyo.
Lakini sisi wananchi hata kule kuthubutu tu kuomba tuone yaliyomo kwenye mafaili hayo hatuthubutu kamwe kuyadai tuyaone.

Lakini, naomba nieleweke, siwatetei wachina hapa.
 
Huu uzi utapata wachanfiaji wachache
Kwa sababu matango pori waliyolishwa hawawezi kuyatapika tena.

Kinachojionyesha wazi kabisa katika mradi huo wa SGR ya Kenya, upigaji mkubwa ulifanywa na wakenya wenyewe, na siyo wachina kama tulivyokuwa tukiaminishwa.

Hapa kwetu ni hivyo hivyo, wapigaji ni hao tuliowapa dhamana ya kuitetea nchi yetu.
 
Back
Top Bottom