nadhani hili suala lipo, na haya ni masuala ya teknolojia kadiri siku zinavyoenda wanadamu tunazidi kutafuta njia za kurahisha mambo zaidi na pengine bila kuangalia ubora au manufaa ya kitu, haswa inapokuja katika masuala ya afya, na hapo ndio tunapotakiwa kuzingatia uzuri na ubaya wa teknolojia.
hili suala limenigusa kweli pana upimaji wa malaria siku hizi nadhani hawatumii darubini wataalam wa fani hii tunaomba mtusaidie, pana kitu wanaita rapi test (nadhani huwa wanakifupi chake) RT kitu kama hiki,
hii imemtokea ndugu yangu, mtoto alikuwa ana homa joto lipo juu sana, kawaida yeye huenda hospital za private, ila siku hiyo akaamua aende ngoja mwananyamala (hospitali ya serikali) kwa kuhisi kuwa pengine angeweza pata huduma nzuri maana siku hizi wanadai pamebadilika,
alienda mwananyama akaandikiwa hicho kipimo RT mara tu akaletewa majibu, akarudi kwa daktari, akaandikiwa sindano ya "kristapen" ikabidi mama aulize kwani ana tatizo gani daktari akamwambia kuwa tumempima malaria hana! hee!! ikabidi mama ahoji sasa hana malaria hii sindano ya nini?? akaaambiwa wewe mpeleke akachome kwa kweli ilibidi abebe mtoto aondoke na ndipo alipoamua kwenda hospitali ya private mtoto akaonekana ana malaria na akaaanza dawa na anakapona, kwahiyo jamani nadhani ni kweli pana vipimo vingie vya malaria mbadala na darubini, tunaomba wenye utaalam watuelimishe!!