Styvo254
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 246
- 227
WanaJamii vipi hali?
Leo nimeona niwajuze kuhusu kupima kiasi/ujazo wa mafuta kwenye gearbox za automatic. Hii ni kwa miundo ya hapo awali inayokua na dipstick ya kupimia. Cha kustajabu ni kua swala hili la upimaji na ujazaji wa haya mafuta ndio limesababisha waunda hii mifumo kuwacha kuweka dipstick za kumwezesha mtumizi wa kawaida kufanya shughuli hii.
Umuhimu wa ujazo sahihi wa mafuta kwenye mfumo ni muhimu kama vile aina na ubora wa mafuta yenyewe. Mambo haya matatu ndio yanayohakiki uhai wa mfumo - hapa nina maana kua uhai ni sawa na utendakazi sahihi. Leo tuhoji mbinu/technique; aina/type na ubora/quality tuangazie wakati mwingine.
La kwanza kufahamu kuhusu mafuta (na vimimini kwa ujumla) ni kua hua yana fura au kuongeza ujazo pasipo na kuongezwa kiasi pale yanapopasha au kuongeza kiasi cha joto. Na pia kuna kiasi maalum cha joto ambapo MFUMO UTENDEA KAZI KWA KAWAIDA - maneno haya tano ni ya muhimu kama injili kwa kuelewa habari hii. Katika hali na mazingira ya kawaida mfumo hua na joto karibia nyuzi tisini sentigred - 90°C. Na kwa kua yale mafuta na maji ya kupooza engine yanagusana kwenye radiator, twaweza kisia kiasi cha joto cha gearbox kutoka na joto la engine tunavolisoma kwa coolant temperature gauge. Muunda mfumo ameiweka alama ile dipstick kulingana na hali mbili; BARIDI - ili kuwezesha usomaji wa awali wa ujazo kwa uwashaji mfumo kwa usalama kama vile baada ya marekebisho au matunzo; JOTO - hali ya kawaida ya matumizi ambayo ndio hali sahihi ya kuchukua kipimo.
Mfumo wa automatic transmission huwa na njia mingi sana za kupitishia mafuta na pia sehemu na makovu mengi ya kudhibiti na kupunguza msukumo wa mafuta katika hali ya utendakazi. Basi ni sahihi kusema, ili kusoma ujazo wa kweli ni muhimu kuhakikisha njia na sehemu hizi zimejaa mafuta na kwa msukumo wa kawaida wa utenda kazi.
Mpaka hapo basi tunaona kua maswala mawili muhimu katika shughuli hii ni Joto na Msukumo wa Kawaida wa utendakazi ili kua na mazingira sahihi ya kuchukua kipimo. Tunapata je kufikia mazingira haya?
Kwa kawaida inapendekezwa kua ukitaka kupima mafuta ya gearbox fata mtindo huu:
1. Washa gari kama kawaida, na ukanyage breki kuzuia gari kutembea.
2. Bila kukanyaga mafuta, tembeza gear lever kwa gear zote pale, ukisimama kwa kila moja kwa sekunde tano hivi; kwanza R, N, D, 4/3...1/L.
MUHIMU SANA KUZUIA KWA SEKUNDE TANO HIVI KWA KILA HATUA ILI GEAR IINGIE VIZURI NA MZUNGUKO UTIMIE
3. Bila kuizima engine weka lever kwa P au N na uweke breki ya kuegesha gari (handbrake)
Katika mda unaochukua kwenda kufungua bonnet, mfumo umesha jaza njia na sehemu zote na pia msukumo wa kawaida kufikiwa ila bado baridi.
4. Chomoa dipstick na uipanguse kwa kitamba safi na kisichotoa nywele. Iingize dipstick tena hadi mwisho wake taratibu.
5. Baada sekunde tano hivi ichomoe tena na uishike umeilaza - yaani mwisho ulioshika na ule mwingine ukiwa sawa toka chini; horizontal kwa Kiingereza.
6. Kwa makini soma yanapofikia mafuta kwa sehemu/kipimo kilichoandikwa COLD/COOL(BARIDI).
7. Ujazo sahihi ni pale mafuta yanapopita Kasoro-Robo ya kipimo lakini chini kidogo ya alama ya kujaa. Waweza pangusa na kurudia zoezi ili kuhakiki.
KUMBUKA HII NI KWA KIPIMO/SCALE YA COLD/COOL(BARIDI)
8. Endapokua mafuta yamepungua, zima engine na ongeza pale pale. Fata mwongozo huu; inachukua lita moja kusongesha level toka alama ya chini, L hadi ya juu, F.
Kama ujazo umezidi, punguza hadi uwe sawa.
9. Baada ya kuweka sawa, endesha gari kwa mwendo wa taratibu umbali wa kilometa moja unusu hadi mbili. Gari au mfumo utakua umefikia mazingira ya kawaida ya utendakazi.
10. Egesha gari mahali sawa, rudia zoezi toka mbili(2) hadi sita(6) safari hii ukisoma kwa kipimo(scale) ya HOT/WARM(MOTO).
Matokeo yako utayasoma vile vile na usahihisho ni ule ule ila utaridia zoezi uengezapo mafuta kwa kua yakuongeza yako baridi.
Utagundua kua kipimo cha Joto kipo juu ya kile cha Baridi ili kukusudia kufura kwa mafuta sababu ya kuongezeka kwa joto.
Ni wazi kua kutozingatia hatua hizi na/au kusoma kutoka kipimo kisicho sahihi kunapotosha zoezi/matokeo. Hii husababisha kupitisha ujazo na hii husababisha kupita kipimo kwa msukumo na kupasua sili na kuleta kuvuja. Hii hudhuru hali ya msukumo wa kawaida na kusababisha mapungufu katika utendakazi.
Transmission za kutoka miaka ya tisini na mapema karne hii hazina dipstick na hutumia njia za kitaalamu za kupima ujazo. Lakini hata pale misingi ni ile ile; Joto na Msukumo wa kawaida.
Happy driving!
Sent using Jamii Forums mobile app