Upinzani Bila Hoja

Joined
Aug 21, 2016
Posts
33
Reaction score
504
Je Upinzani wa aina hii una tija kwa watanzania ?

Kwa muda sasa, kwenye mitandaoya kijamii kumekuwepo na mawazo mbalimbali kuhusiana na masuala kadhaa yanayohusiana na nchi yetu. Nimeona ni vyema nitoe maoni yangu kuhusu mambo yafuatayo.

Kwanza nianze na hili linahusu maoni ya kejelina ya kupotosha yanayotolewa na baadhi ya watanzania ambao nadhani ni wa upande wa upinzani ambao wanakejeli au kudhihaki hatua zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya tano kuhusu hasa kuleta ndege za kubeba abiria. Ikumbukwe, kwa muda mrefu nchi yetu haikuwa na ndege za kubeba abiria. Hali hii haikuipa sifa nzuri nchi yetu, hasa nje ya nchi.

Serikali ya awamu ya tano kwa muda mfupi imeweza kununua ndege za abiria. Na imeweza kufanya hivyo bila kuomba msaada kwa wahisani na imelipa wala haikukopa.

Ni jambo la kuisikisha kuona kuna watanzania ambao wanaumizwa na hatua hizi zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya tano. Watanzania hawa wamekosa hata chembe ya uzalendo na kuona jambo hili ni heshima kwa nchi na wala si heshima ya CCM tu. Mawazo ya namna hii ni aibu, na upinzani wa namna hii hauna tija kwa watanzania.

Jambo lingine ninaloliona kwenye mitandao, ni la safari za nje ya nchi hasa kwenye mikutano ya Taasisi za Kimataifa kama UN, World Bank, World Trade Organization, IMF na kwenye nchi za Ulaya, Marekani au Mashariki ya Mbali kama Urusi, China Japani na India. Upo mtazamo wa watanzania wachache na nadhani ndugu zetu wa upinzani ambao wanaona kwenda kwenye mikutano hiyo kwa viongozi wa juu wa nchi yetu ni suala la lazima na heshima sana kwani wanadhani huko ndiko kwenye majibu ya matatizo ya nchi yetu.

Wapo watakaokubaliana na mimi kwamba Taasisi nyingi za kimataifa zilianzishwa kwa ajili ya kulinda maslahi ya nchi zilizoendelea na siyo maslahi ya nchi zinzaoendelea kama Tanzania. Tukumbuke Taasisi hizo zimetoa misaada mingi sana Afrika na Tanzania ikiwemo lakini misaada hiyo ilikuwa na masharti mabaya sana ambayo imesababisha nchi nyingi zilizotegemea misaada hiyo kumebaki tegemezi.

Hivyo basi kulingana na sababu niliyoileza hapo juu, matatizo ya nchi yetu hayatatatuliwa kwa viongozi wetu kwenda kushiriki kila mikutano itakayoitishwa na taasisi hizo nilizozitaja au kwenda mara kwa mara kwenye mikutano inayoitishwa na Marekani, Ulaya au nchi za Asia. Nadhani niko sahihi kusema majibu ya matatizo ya nchi yetu tutayatatua sisi wenyewe kwa kuwa na uongozi bora wenye kujituma unaotanguliza maslahi ya watanzania na kuhakikisha raslimali zetu zinatuka vizuri kwa manufaa ya watanzania.

Serikali ya awamu ya tano imeonyesha dhahiri ina nia ya kuondokana na utegemezi uliokuwepo na inaonyesha inayo dhamira ya kuhakikisha kwanmba raslimali za nchi yetu zinatumika kuleta maendeleo ya watanzania. Hivyo kupunguza safari za nje kwa viongozi wa awamu ya tano ni dalili nzuri inayoonyesha kwamba majibu ya matatizo ya nchi yeetu tutaweza kuyatatua watanzania wenyewe.

Aidha, miaka michache iliyopita upinzani ulipiga kelele sana kuhusu safari za nje zilizofanywa na viongozi wa awamu ya nne. Upinzani ulisema hakuna tija kwa safari hizo na wakakokotoa fedha zilizotumika. Leo, Upinzani huo huo unalalamika kwamba viongozi wa serikali ya awamu ya tano ni wazito kwenda kwenye mikutano ya nje. Upinzani huu sioni kama una ajenda ya maana zaidi ya kuwapotosha watanzania na nadhani upinzani huu unaongozwa na chuki na inda na sidhani kama unatija kwa watanzania. Ashakumu si matusi.
 
Wewe Mzee unamalizia Maisha yako ya siasa kwa aibu ya njaa sana. Hivi kuna watu wengine hamuwezi kuishi bila kutegemea incentives za gvt. Mbona wengine wazazi walemavu na wanalima na wametusomesha.

Fikiri upya wa jina
By Fred
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…