Upinzani kufanya maandamano siku tatu mfululizo kuanzia Jumatatu

Upinzani kufanya maandamano siku tatu mfululizo kuanzia Jumatatu

Kenyan

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
414
Reaction score
314
Seneta wa kaunti ya Nairobi Edwin Sifuna kwenye mahojiano na televisheni ya Citizen amethibitisha maandamano sasa yatadumu kwa siku tatu mfululizo kila wiki; kuanzia Jumatatu mpaka Jumatano.

Tangazo hili linakuja huku taifa likikadiria hasara kubwa kufutia maandamano makubwa yaliyofanyika Jana ambapo sehemu ya barabara maarufu ya 'Nairobi Expressway' iliharibiwa na waandamanaji.

Kwa upande mwingine Waziri wa usalama wa ndani Professor Kithure Kindiki amesema kuwa mamia ya watu akiwemo Mbunge mmoja ambaye hakutaja jina wamekamatwa na polisi kwa kuongoza maandamano.

Ikumbukwe Jana tu Muungano wa sekta binafsi Kepsa ulisema kuwa taifa linapata hasara ya takriban bilioni 3 , sawa na trilioni 52 za Tanzania Kila siku panapotokea maandamano.

Rais William Ruto bado hajanena lolote kuhusu maandamano ya Jana ambayo wengi wanahisi yalikuwa ni makali kuliko ya hapo nyuma.
 
Back
Top Bottom