Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Familia ya Walz inaonekana kuwa na mgawanyiko mkubwa wakati ambapo mgombea mwenza wa Kamala Harris, Tim Walz, ambaye ni Gavana wa Minesota anajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa 2024 huko Marekani. Jeff Walz, kaka mkubwa wa Tim na mfuasi mkubwa wa Donald Trump, ametoa msimamo wenye nguvu dhidi ya ndugu yake.
Jeff, mwenye umri wa miaka 67, amesisitiza waziwazi kuwa hatamuunga mkono Tim na kamwe hatakubali sera zake. Kwa mujibu wa taarifa, Jeff amepinga sera zote za Tim kwa asilimia 100%, akieleza kuwa kaka yake hafai kuwa na mamlaka juu ya mustakabali wa watu. Msimamo huu wa Jeff umejiri katika hali ya kukata tamaa ya kisiasa, huku akipendelea kuunga mkono Trump badala ya tiketi ya Harris-Walz.
Hata hivyo, baada ya kuingilia kati kwa dada yao Cathy Walz Dietrich, ambaye amemtaka Jeff atulize pupa kutokana na kauli zake dhidi ya Tim, Jeff amekubali kupunguza ukosoaji wake wa hadharani.
Mama yao, Darlene Walz, mwenye umri wa miaka 89, pia ameonyesha matumaini kwamba mgawanyiko huu wa kifamilia unaweza kupungua kupitia juhudi za Cathy.
Soma ==>Tim Walz Gavana wa Minesota ateuliwa kuwa Mgombea Mwenza wa Kamala Harris
Soma ==>Tim Walz Gavana wa Minesota ateuliwa kuwa Mgombea Mwenza wa Kamala Harris