Upinzani sio uadui, watu makini wa upinzani wanaweza kutumiwa na Rais

Upinzani sio uadui, watu makini wa upinzani wanaweza kutumiwa na Rais

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
441
Reaction score
1,065
Nchi ni ya watanzania wote bila kujali vyama vyao wala chochote

Rais akishaapishwa anakuwa kiongozi wa nchi sio wachama hivyo anakuwa kiongozi wa watu wote

Kwa msingi huo watu wote ni mali ya Rais na wanayo nafasi sawa mbele ya Rais bila kujali itikadi zao

Vyama vya upinzani vina watu wengi wenye mawazo mbadala ambayo pengine yakitumiwa yanaweza kuleta matokeo chanya kwenye nchi yetu

Watu kama Tundu Lisu, Zitto Kabwe, J.J Mnyika, G.Malisa, Yericko Nyerere na wengine wengi wote ni mali ya Rais

Hivi haiwezekani watu wa aina hii wakatumiwa rasmi na TISS wakapewa jukwaa rasmi la kukutana na kushauri moja kwa moja kwa Rais

Faida itakayopatikana ni kuwa wataongea bila unafiki, bila uchawa, bila kujikomba, bila woga wala wasiwasi wowote hivyo kutoa uhalisi wa ilivyo na inavyotakiwa kuwa
 
Back
Top Bottom