Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi wine amewatolea mwito raia nchini Uganda kuandamana kwa amani na bila ya silaha kumpinga rais Yoweri Museveni aliyetawala taifa hilo kwa karibu miongo minne.
Akizungumza kwenye makao makuu ya chama chake cha National Unity Platform (UNP) mjini Kampala Wine amesema muda umefika kwa umma kuandamana dhidi ya Museveni aliyeigia rasmi mamlakani mwaka 1986.
Jeshi la polisi limeonya kuhusiana na mwito huo na kusema halitasita kumkamata na kumfungulia mashitaka yoyote atakayeshiriki maandamano hayo na shughuli zozote za kinyume cha sheria.
Kulifanyika maandamano mwezi Novemba ya kupinga kukamatwa Wine, yaliyotawanywa kwa nguvu na vikosi vya usalama na kusababisha vifo vya watu 54.