SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Katika kile kinachoelezwa ni kujipanga kwa vyama vikuu vya upinzani nchini kuelekea uchaguzi mkuu 2020. Kumekuwepo na mazungumzo ya Ndugu Zitto Kabwe Kurejea Chadema na Maalim Seif Shariff Hamad kuhama CUF na kujiunga na ACT Wazalendo kwa malengo kuwa muungano wa vyama vya upinzani umsimamishe Zitto Zubeir Kabwe kuwa mgombea wake katika nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema na Maalim Seif Shariff Hamad kama mgombea wa makamu wa Rais kwa tiketi ya ACT Wazalendo.
Muswada wa sheria ya mabadiliko ya vyama vya siasa nchini kupitishwa kuwa sheria na Freeman Aikael Mbowe Mwenyekiti wa Chadema Taifa na KUB kuwekwa mahabusu kwa siku takribani 97 sasa vinatajwa kutibua mipango hii. Kwani kwa sheria hii sasa yeyote atakayehama sasa hawezi kuwania nafasi yoyote katika uchaguzi mkuu ujao kwani sheria hiyo inamtaka anayehamia chama kingine apate haki ya kugombea katika nafasi za dola kama uenyekiti wa mtaa au kijiji, udiwani, ubunge au urais baada ya kukaa kwenye chama kipya miaka miwili kwanza.
Baada ya yote haya dua na sala ni kwa kesi ya CUF inayosubiri hukumu. Wengi wao wakionekana kumuombea mabaya mwenyekiti wa sasa wa CUF Prof wa uchumi Ndugu Ibrahim Haruna Lipumba kushindwa kesi hiyo dhidi ya katibu mkuu wake Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad ili iwe rahisi kutengeneza kolabo waliyoikusudia.
Malengo ya upinzani kwa sasa si kushinda nafasi ya urais bali wanahitaji kumsimamisha mgombea atakayeweza kuwaongezea idadi ya viti vya ubunge hadi kufikia asilimia 40-45 kati ya wabunge wote ndani ya Bunge ili kuweza kuisimamia, kuibana na kuishauri serikali.
Mwisho mengi zaidi yanasubiriwa ni baada ya Mbowe kutoka gerezani ambako mara kadhaa Ndugu Zitto amekuwa akimtembelea na kufanya naye mazumgumzo ya kina na faragha huku ikisadikiwa kuwa ni mipango kuelekea 2020. Inasadikika ipo mikakati ya kumdhibiti Ndugu Tundu Lissu aache kuitaka nafasi ya Urais au uenyekiti ndani ya Chadema.
Sent using Jamii Forums mobile app