Upishi wa Bagia za Dengu

Jade_

Senior Member
Joined
Apr 19, 2015
Posts
122
Reaction score
214
Habari zenu, natumai mpo salama. Mara ya mwisho nilitengeneza white sauce na leo napika bagia za dengu.

Ukitaka kuangalia video ya haya mapishi unaweza kuangalia hapo chini. Ukipenda unaweza “kuilike” hiyo video, “kusubscribe” kwenye channel yangu na kuangalia video nyingine.

Tuanze mapishi.

Mahitaji ya Bagia za Dengu
400g unga wa dengu
2 tsp (kijiko cha chai) hamira
Mafuta ya kupikia (kuchanganyia kwenye mchanganyiko na ya kupikia)
Chumvi
Maji au maziwa (yawe vuguvugu yanayokaribia kuwa moto )
Karoti, hoho pilipili au viungo uvipendavyo

Nilianza kwa kuchekecha unga wa dengu, hamira na chumvi kwenye bakuli. Nilivyomaliza niliweka mafuta na maji taratibu, huku nikikukoroga mpaka mchanganyiko ukawa mwepesi kiasi. Nikaufunikia na kuacha hamira ifanye kazi kwa masaa 2.

Nikichekecha mahitaji yangu makavu


Mafuta kwenye mchanganyiko


Nikikoroga mchanganyiko


Mchanganyiko uliofunikiwa kwa ajili ya hamira kufanya kazi


Wakati nasubiria hamira ifanye kazi nilianza kuandaa viungo vyangu (karoti, pilipili na hoho) kwa kuosha na kuvikatakata vipande vidogo.

Nikiosha viungo


Nikikatakata viungo


Karoti, hoho na pilipili vimekatwa katwa


Masaa 2 yalivyoisha, nilichanganyia viungo kwenye mchanganyiko wa unga na kupasha mafuta kwenye karai kwa ajili ya kukaanga bagia. Mafuta yalipopata moto nilikaanga bagia, kwa kumwagia mchanganyiko kwenye mafuta na kijiko.

Mchanganyiko ukiwa tayari


Mchanganyiko baada ya hamira kufanya kazi


Nikichanganyia viungo kwenye mchanganyiko


Nikipasha moto mafuta


Nikichota mchanganyiko kwa ajili ya kukaanga


Nikimwagia mchanganyiko kwenye mafuta


Nilikaanga bagia mpaka zilivyopata rangi ya brown yenye unjano kwa mbali.

Nikikaanga bagia


Nikitoa bagia jikoni zikiwa tayari


Bagia zikiwa tayari


Bagia iliyokatwa kwa ukaribu


Bagia za dengu
 
Daah nazipenda hizi, ila home wanazikosea kuzipika, kuna mpemba mmoja huwa anazipika tamu mno.
 
Nauliza.
Wapi kuna soko la Dengu?
Kilo moja ya Dengu inauzwaje ?
 
Unga wa Dengu nanunua soko la Majengo hapa Dodoma. Bei yake sikumbuki vizuri maana muda umepita.
Ila Dengu sijui nadhani ukiulizia sokoni watakuelekeza.
Dah!
Kumbe Dodoma kuzuri hivi, kuna misosi yote!
Au nyumbani kwako tu 🙂?
Aisee, bajia zinaonekana tamu kweli
Asante kwa ujuzi, nikamkurupue huyu chumbani kazi kuangalia netflix tu....
 
Dah!
Kumbe Dodoma kuzuri hivi, kuna misosi yote!
Au nyumbani kwako tu 🙂?
Aisee, bajia zinaonekana tamu kweli
Asante kwa ujuzi, nikamkurupue huyu chumbani kazi kuangalia netflix tu....
Ndio, Tanzania nzima kuna misosi.
Hata wewe unaweza kujipikia bagia nzuri ukifuata maelekezo niliyotoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…