Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe tuko wengi namimi pia ni hivyo hivyo lakini mwenzio taste yake inanishinda na sijui swali la huyu jamaa anamaanisha namna ya kuyapika yakiwa makavu au mabichi,mbona ni rahisi sana kuipika mboga yeyote ya majani.Kama ni makavu chukuwa vitunguu uvikatekate na nyanya na kama ni mtumiaji wa pili pili weka mbichi moja na tena weka mafuta ktk sufuria yako then anza kuvikaanga hivyo vitunguu pamoja na nyanya mpaka vibadilike rangi then itupie mboga yako ndani ya hilo sufuria uichanganye na kwa pamoja na hivyo vitunguu na nyanya zilizoivya changanya kidogo kidogo na mwiko wako na halafu ongeza maji kidogo na kama una stock yeyote aidha ya kuku au nyama yenye chumvi ndani yake ongezea ili upate mchuzi na kama unayo tomato paste pia unaweza tia ili upate chuzi zito,weka lid juu ya sufuria halafu punguza moto ili iive pole pole kwa moto mdogo,mboga yako tayari kwa kulia na ugali bona apetit!!.Mr Msherwampamba:canada:Yaani katika mboga ambazo sizipendi hayo majani hayo majani siyapendi...ni bora nile ugali kwa chumvi...kuliko kula ugali na hayo makitu hasa ile migingi yake ya nyuma dahh.......
Mama yangu ndiyo analipika hivyo hivyo. Yeye anaweka na pili pili pia.Chukua tembele lichambue vizuri halafu liweke kidogo juani ili lisinyae kidogo(sio lazima) baada ya hapo weka kikaangio chako tia vitunguu ndani ya mafuta then nyanya kisha tembele.Usifunike maana litakua na maji maana ya ule mvuke wa kufunikwa