Upo tayari kuvumilia mateso kiasi gani usimwambie rafiki yako msaliti sehemu ulipoficha shilingi bilioni 2

Upo tayari kuvumilia mateso kiasi gani usimwambie rafiki yako msaliti sehemu ulipoficha shilingi bilioni 2

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Ni vitu vinavyotokea kwenye maisha ya kweli, sio kwenye muvi tu, bilioni 2 ni lugha ya kimafumbo ya kiasi kikubwa cha fedha kwako kinachoweza kubadili maisha yako.

Hio ni siri yako ambayo rafiki yako anaijua kwa juu juu hajui ulipozificha pesa.

Ghafla rafiki anaingiwa tamaa ya usaliti anataka pesa hizo zote ziwe zake.

Anakuja nyumbani kwako kirafiki wala huwezi kumdhania yupo na mawazo yapi, anaweza tumia mbinu kibao kama kukuwekea dawa ya usingizi mzito kwenye kinywaji, kuzuga anaenda chooni kisha anakupiga na kitu kizito kisogoni unapoteza fahamu, n.k.

Unaamka ukiwa umefungwa na kamba kwenye kiti.

Huamini unachokiona, uliemdhania rafiki anakuuliza "NAHITAJI HIZO PESA SHILINGI BILIONI 2 ZIPO WAPI ?"

Mateso utatopewa ni kama:

kupigwa vibao vizito
ngumi / knuckles
viboko, kupigwa na mkanda wa ngozi

Ukidanganya zilipo fedha adhabu zinazidi

Upo tayari kuvumilia mateso kiasi gani kufumba mdomo
 
Vyovyote vile utoe siri ama uache mwisho atakuua.

Toa tu siri, ili akuue. Hiyo hela akichukua itasaidia watu wengi.
 
Huyu ndio yule stelingi mwenye mawe anakimbiza jamaa mwenye bunduki 😂😂😩, kuitwa chizi sio lazima uokote makopo
 
Back
Top Bottom