Askari Mstaafu: Sijalipwa stahiki zangu, Polisi wamenipa Siku 7 nikabidhi nyumba la sivyo vitu vyangu vitatolewa nje

Askari Mstaafu: Sijalipwa stahiki zangu, Polisi wamenipa Siku 7 nikabidhi nyumba la sivyo vitu vyangu vitatolewa nje

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056

Mzee John Samwel Swai(61) mstaafu wa Jeshi la Polisi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia asiondolewe katika kambi anayoishi kwani bado hajalipwa fedha za mizigo pamoja na fedha za likizo ambazo anapaswa kulipwa.

.Mzee huyo alistaafu mwaka 2020 baada ya kutumikia jeshi la polisi kuanzia mwaka 1983 amedai kupewa barua na Mkuu wa Kambi za Polisi inayomtaka kuhama ndani ya siku saba kuanzia Februari 04 mpaka leo Februari 10 na endapo asipohama vitu vyake vitatolewa nje.

Kupitia barua aliyopewa tarehe nne mwezi huu imesema “Umeariwa kukabidhi nyumba tajwa hapo juu, kwani umeshastaafu kazi toka 2020.

Oc Barracks amekuamuru kukabidhi nyumba tajwa hapo juu kwa kuwa umestaafu kazi. Umepewa siku 07 kuanzia leo tarehe 04/02/2025 hadi 10/02/2025 uwe tayari umekabidhi nyumba hiyo, Kushindwa kutekeleza amri hii, vitu vyako vitatolewa nje, hivyo unaamriwa kuviondoa mwenyewe kabla ya kutolewa”

Mzee Swai amewaomba wasaidizi wa Rais ambao Jeshi la Polisi lipo chini yao akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kumsaidia wakati huo serikali ikiendelea kushuhulikia malipo yao.

Jambo TV imefanya jitihda za kumtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime kwa njia ya simu lakini jitihada hazikuzaa matunda.
 

Attachments

wakiwa madarakani sasa, huwa wanasahau kama Kuna kustafu na watakuja kuishi uraiani huku huku, watakutana na wale waliowasingizia kesi, Raisi yuko bize na mambo mengine
Hao wadogo wadogo Huwa wanatumia tu kutekeleza amri za wakubwa zao
 
Mzee John Samwel Swai(61) mstaafu wa Jeshi la Polisi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia asiondolewe katika kambi anayoishi kwani bado hajalipwa fedha za mizigo pamoja na fedha za likizo ambazo anapaswa kulipwa.


Dr. Samia alipoingia madarakani kama Amri Gesi mkubwa alionyesha wazi kabisa kutokupenda Gesi la Furushi .
Akaunda na Tume ya Aki jinai .
Katika tume sidhani kama walizungumzia haki za polisi zaidi ya haki za washutumiwa.

Baada ya kunogewa na mauzo ya Bandari anatamani kusalia madarakani kwa namna yoyote . Wakora wa mambo na wahuni wa uchaguzi wakamwambia bila Poorishi hushindi . Anajifanya kuwa anadapenda baadhi ya maafisa wakubwa lakini wale kule chini bado akawa na walakini nao japo anataka ushindi wa mezani .


Nchi ikiwa na kiangozi asiye na maono ni hatari sana . Katika mapolisi hao hao kuna wanaopata haki zao na wanaokosoa .
Tuo maana Katiba ya Jaji Warioba ilipendekeza pawe na Tume maalumu inayosikiliza Malalamiko na kutoa haki kwenye Jeshi la polisi.

Nyumba ya serikali na mastaafu wa Jeshi kuna haraka gani ya kumfukuza kwenye nyumba wakati amevumilia kucheleweshwa na haki zake . Kama wanaharaka basi waharakishe na stahiki zake .
Bila shaka kuna rushwa pia kwa mtu mwingine anayetaka nyumba hiyo .

Wakati mwingine mifumo mibovu na utawala Corrupt unabipuuza sana vyombo vya dola . Mfano ni Kongo askari wa Kongo ni hopeless kabisa bora hata wa Burundi .
Lakini yote ni kwa sababu Serikali ya wakongo haitaki kuwajibika kwa wananchi na kulinda mali zao umma hivyo haina haja ya kuwa na askari waadilifu wenye kusimamia haki . Matokeo yake wananchi wanaichukia serikali na kujiunga na waasi .
Ndio maana nchi za kisini mwa jangwa la Sahari zote zinatunza majeshi yake kupitia misheni za UN zinazofadhiliwa na Marekani na wakora wengine na wezi wa rasilimali za dunia . Mfano Burundi au hizi nchi nyingine za mashariki siku vita ya Kongo na Sudani ikiisha . Je,serikali imejipanga kuwapa wanajeshi wake mishahara inayokidhi maisha yao mabeli na sasa wananufaika na mishahara ya UN . ?

Seikali iweke wazi stahiki za watumishi wake na wale wanaozikanyaga ndio washughulikiwe sio kuwadhalilisha walionyimwa haki zao.

Lakini pia ni wakati sasa wa Vyama vya siasa mwaka huu kwenye uchaguzi kuja na sera za makazi ,ardhi, Misitu ,madini ,gesi , Utalii, ajira , Bima ya afya kwa wagonjwa , Elimu ya umma , Uwanda na teknolojia , Kilimo na biashara na haki kwa kila mtanzania bila kutishiwa kuuawa au kutekwa au kufukuzwa kazi au kufilisiwa mali kwa sababu tu ya tofauti za kimitazamo kwa wananchi .

Bila shaka Tundu Lisu na ACT watajipanga vya kutosha kuja na sera zenye kuwavutia mpaka wale wanaoilinda CCM na kujua kua CCM kina wenyewe na wenyewe sio hao mapolisi wasio na thamani kwenye chama baada ya kustaafu.
 
Back
Top Bottom