SimbaMpole123
JF-Expert Member
- Apr 23, 2023
- 5,501
- 4,956
Mi Kama Simba mpole, naomba niongolee suala la uponyaji wa kimiujiza(faith healing).
Hili suala limefanyiwa utafiti na watu psychology na kugundulika Ni kitu Cha uongo na utapeli na mpaka Marekani watu wanafanya na kufaidika kununua mandege na kujenga mahoteli makubwa.
Cha kwanza, mtu akiitwa pale mbele kwa mfano, anakuwa na Ile andrenaline rush, hata Kama anaumwa kwa kuwa akili yako unataka upone kimiujiza, utahisi umepona ili usiangushe Imani yako na usimwangushe yule mchungaji mbele za watu na ukisema umepona watu wataamini ni kweli lakini unashangaa ukirudi we ni mtu yuleyule ndo biolojia ya binadamu ilivyo lakini tayari watu wanajua umeponywa.
Cha Pili, Magonjwa ambao hawa wachungaji wanasema wanaponya ni magonjwa yasioonekana, ukimwi, kisukari, tumbo sijui, mtu kutotembea, lakini magonjwa yanayoonekana kama mtu aliyekatwa mguu, mapacha walioungana, mtu mwenye dwarfism (kuwa mdogo Sana), na mengineyo ambayo mtu huona kwa macho hawawezi tibu na wakijaribu wanafeli mbele za watu.
Kama kweli Mungu anaponya kwanini anachagua magonjwa fulani na anaacha mengine, yeye si mweza yote ama. So Ina maanisha pale makanisani ni acting tu na njama za kujitangaza kibiashara na kuchukua mabillion ya hela za watu maskini kwa kutumia Imani zao potofu kujiendeleza kibinafsi.
Cha tatu na cha mwisho, Mimi sijui kwanini watanzania wengi mmeingia kwenye hilo janga, yaani mtu hujui unakula nini kesho, au unalala wapi umepata hela kidogo kwa shida unaenda kumjengea mtu hoteli, kweli?
Kisa yeye kaamka kavaa suti kaingia kanisani na kusema kuwa ye ni Mtumishi wa Mungu, na kaweza kuaktisha watu wajifanye wanaumwa ili wewe uendelee kumtumikia kwa kumtajirisha na wewe unakubali.
Mungu kama yupo ni mahala kote yupo, atakutokea hata wewe. Ila wewe unamwamini mtu aliyesema yeye ni mtumishi wa Mungu na we unampa tu hela zako, hata Yesu hakuwa hivyo, hakuwa na maghorofa, mafarasi, alikuwa wakawaida.
Bill Gates ambae haamini Mungu ametoa msaada mkubwa duniani kuliko hao wezi wanaotumia Imani potofu za watu kwa faida zao binafsi.
Fikirieni hili suala, tujiendeleze kifikra, Afrika tunaanguka hapa tu, wenzetu washajitoa huku.
Umaskini wa kimawazo ndo umaskini mbaya kuliko wote.
Asanteni.