Upotevu wa Watalii mapango ya Amboni 1970

Upotevu wa Watalii mapango ya Amboni 1970

Heri lee

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
981
Reaction score
537
Kwema ndugu....

Mnamo mwaka 1970 tarehe 5-8 watalii kutoka nchi Ujerumani waliingia nchi Tanzania Donald Morison na mkewe Abe kufanya utalii binafsi jijini Tanga wakiwa na mbwa wao kama wazungu wengi wapendavyo kutembea na mbwa

Siku ya tukio

Mwezi wa 9 mwaka huo 1970 watalii Donald na mke walitua jijini Tanga kufanya utalii huko pangoni Amboni walipofika uongozi wakijiji huo walipokewa na baraka zote wakapewa

Masharti Pangoni
Ilikuwa ni sharti kuwa mila na desturi za mapango hayo hairuhusiwi kuingia na mnyama yeyote kwa ulinzi binafsi k.v mbwa mzee ambaye alikuwa eneo lile akidai kuna mizimu ya mabavu umbo LA joka lisiloruhusu kuingia humo na mbwa
Kwa wale waliobaatika kufika Amboni wanajua eneo LA kufanyia tambikk LA mizimu huko ndani ya mabango eneo lenye uwazi Fulani""

Wagoma kuacha "Mbwa""

Watalii hawa waligoma kabisa kuacha mbwa wao kama mlinzi wao kuangalia maajabu haikuwa sababu ya kuzuia kuingia na mbwa huyo pangoni(kama ujuavyo ngozi nyeupe zinavyofanya lolote kwa wakati ule)

Waingia pangoni wavunja amri ya Mizimu

Baada ya kuingia na mbwa yule kama mlinzi hawakuonekana tena kwa siku kadhaa haikuwa kawaida kukaa muda mrefu huo ilipita wiki 2 bila Donald na Abe kuonekana

Wafuatiliwa nyayo

Ndugu zao kutoka nchini German na uongozi was kijiji wakaingia pangoni kutafuta watalii

Je Donald yuko wapi na mkewe na mbwa wao??
Twende pamoja...
Wakifuatilia nyayo zao ziliishia kwenye miamba pasipo weza onekana

Kofia ya Donald

Kofia ya Donal iliokotwa eneo ambalo linajulikana kama USA lenye sanamu ya MTU alieshika mwenge kama yule wa
Washington DC

Zaidi ya hapo haikupatikana lolote licha ya utafiti kufanyika zaidi ya miezi 5 haikupatikana hata unyoya

Nini kiliwapata??

Mwezi wa 6 mwaka 1971
Haifaa utafiti wote ukagonga mwamba
Lakini walikufa au walipotea kimiujiza?
Wataalamu walitumia mbinu ya ,unyayo footsteps
Kwa njia ya biometric lakini waliishia kufika umbali wa mita kama 120 hivi ni haikuonekana chochote utafiti ukaishia hapo

Mbwa aonekena Kilimanjaro

Udhibitisho kuwa kuna njia kutoka mapango ya Amboni hadi miteremko ya mlima Kilimanjaro (m 5895) ulifikia kuaminika baada mbwa kuoneka Kilimanjaro miezi 7 baada ya kupotea kwa Watalii baada ya utafiti iliaminika mbwa huyu ndie alieingia pangoni na watalii hadi kufikia hapo ndugu walitengeneza mfano wa kaburi na kuihifadhi kofia ya Donald

Hadi Leo hii wajulikani walipo hadi miili yao
 
Duuuh.kuna choni ano.

Ova zaramo empire nawasilisha
 
Inavyosemekana walitaka kuongozA na mbwa anatosha
 
Pale unaweza kuruhusiwa kuingia bila muongozaji? Sijaona muongozaji akitajwa na yeye kupotea.

Ndani ya hayo mapango kuna eneo lazima utembelee magoti na unapita mtu mmoja mmoja. Kuna giza wakati wa mchana, sijui usiku inakuaje.

Kuna shimo ukifika sehem wanasema ndio inaaminika hao wazungu walipotelea hapo huku wengine wakidai linatokezea Kilimanjaro.

Hii habari imeghubikwa na sintofaham nyingi sana.
 
Pale unaweza kuruhusiwa kuingia bila muongozaji? Sijaona muongozaji akitajwa na yeye kupotea.

Ndani ya hayo mapango kuna eneo lazima utembelee magoti na unapita mtu mmoja mmoja. Kuna giza wakati wa mchana, sijui usiku inakuaje.

Kuna shimo ukifika sehem wanasema ndio inaaminika hao wazungu walipotelea hapo huku wengine wakidai linatokezea Kilimanjaro.

Hii habari imeghubikwa na sintofaham nyingi sana.
Nakubaliana na wewe mkui
 
Nadhani pale sayansi inaposhindwa kufanya kazi ndipo imani inatoa majibu rahisi na hitimisho ya mambo kama haya. Siamini kama mizimu au matambiko ndio chanzo cha kupotea kwa watalii.
 
Tatizo letu ni moja huwa historia hatuiweki sawa maana tukio lililotokea na za kutunga hatuzijui

Hii historia niliisikia zamani wakisema mbwa alionekana Mombasa
Na baada ya awamu hii atakuwa kaonekana pemba
Kuhusu hii michoro kama ya statue of liberty wanasema nayo ilichorwa zamani sana enzi na enzi
Kuamini haya lazima ujtoe ufahamu kabisa au uwe kichaa kichaa
 
Asante kwa kutupa simulizi,nimesoma lkn namna ya uandishi wako duh!.

Hiyo mizimu itakalia kudaba vimtu lkn tunahistoria mbaya ya utumwa na kuendeshwa hovyohovyo!,hayatusaidii lolote zaidi ya mikwala ya kuogofya!.
 
Back
Top Bottom