Nilimsikiliza vyema mheshimiwa rais katika hotuba yake kuhusiana na Corona alipokuwa akimwapisha waziri Mwigulu.
Waziwazi mheshimiwa rais alipotosha kwa makusudi katika maeneo kadhaa labda kwa maslahi zaidi ya kisiasa. Kwa bahati mbaya gonjwa hili halihitaji propaganda za kisiasa bali ufumbuzi pekee wa kisayansi:
1. "Wanasema ni lockdown, watapata wapi chakula wanachopata masokoni. Kwenye lockdown, masoko nayo yatafungwa. Watakosa chakula maana hawana mashamba."
Huu ni upotoshaji wa makusudi kwani hata kwenye total lockdown, sehemu za muhimu kama za manunuzi ya vyakula huwa wazi. Huwa kuna taratibu tofauti tofauti kutegemeana na mahali, ambapo kwingine wachuuzi huuza kwa zamu ili kuzuia mikusanyiko, nk.
2. "Wanasema ni lockdown wakati wanaendesha ma STK. Wanajua hata hiyo mishahara yao inatokana na kodi. Watakula wapi?"
Huu ni upotoshaji mwingine wa wazi kujaribu kuweka mwonekano batili kuwa katu serikali haziwajibiki kwa lolote kwenye majanga.
3. "Nimeongea na marais Ramaphosa na Museveni. Huko walikokuwa na lockdown wanalia. Wamekufa maelfu 50+ kwa njaa na hivi wako kwenye kuachana na hizo lockdown."
South Africa wako kwenye hatua za kumaliza iliyokuwa total lockdown na Ramaphosa alikuwa wazi tokea mwanzo, kuwa heri waende kwenye total lockdown mapema kuliko baadaye maana ingewagharimu zaidi in terms of maisha ya watu na hata raslimali kwa baadaye kama wakichelewa. Walienda lockdown wakiwa na wagonjwa chini ya 200. Sasa kasi ya maambukizi imedhibitiwa.
South Africa walikuwa wanagawa chakula bure kwa wahitaji. Ugonjwa umedhibitiwa kwa ujumla, kwani kasi ya maambukizi wamesha idhibiti na sasa wanarejea pole pole kwenye maisha yao ya kawaida.
Uganda walikuwa kwenye partial lockdown waliyoianza mapema mno. Case zao zote muda wote zimekuwa ni imported. Hawakuwa na maambukizi ya ndani kabisa. Wao si vifo vya Corona tu, bali hata vya njaa navyo hamna.
Ugonjwa wameshaudhibiti na wanarejea pole pole kwenye maisha yao ya kawaida.
Wapi huko Meko alikuwa akidai maelfu wamekufa njaa kwenye lockdown? Tumepigwa changa la macho. Si mbaya akijua kuwa hawezi kuwadanganya watu wote siku zote.
4. "Sampuli mbalimbali za kware, kondoo, mbuzi, oil nk, kuwa na majibu hata positive au negative".
Sampuli zinaweza kuwa contaminated (cross contamination). Bila ya kujua handling ya sampuli ilikuwa je, tokea kwenye source hadi mrejesho wa majibu, labda kama handlers ni malaika; vinginevyo si sahihi kuwa na tuhuma nzito za sabotage kama zile alizozitoa kwa wote. Ila kama ni hawa wasiojulikana ndiyo wenyewe handlers wa hizo sampuli (katika hatua yoyote), hawa ambao wao hata risasi hukata kona, mbona kuwaamini yahitaji moyo wa ziada?
5. "Kila kifo si lazima ni Corona".
Hivi ni kifo kipi walichothibitisha kuwa ni cha Corona? Anapendekeza hadi maiti ivalishwa PPE ili kusafirishwa, kama vile wauguzi wenyewe wanazo hizo PPE za kukidhi mahitaji yao.
6. "Dawa inapatikana Madagascar, tutatuma ndege ikalete".
Dawa inayosemekana Madagascar ni mitishamba. Nayo ni kama hii hapa. Haya ya hivi yanapatikana maporini kote. Makabila mbalimbali wanaita majina yake. Huu unaitwa Tetradenia riparia:
Inahitaji ndege kufuata haya ya namna hii Antananarivo? Au labda ilikuwa mahsusi kwa ajili ya wapiga nyungu kuwaonyesha yuko busy kutafuta ufumbuzi?
7. Nk nk.
Yaonyesha hotuba ile ililenga katika kuleta confusion ile ile inayopigiwa chapuo kwa bidii na wale waimba mapambio na mavuvuzela yao. Huku tukibakia pale pale kwenye acha wenye kufa wafe, wa kuishi waishi hadi tiba au chanjo itakapopatikana.