Upotoshaji mkubwa unaofanywa kwenye Elimu ya Ujasiriamali

Upotoshaji mkubwa unaofanywa kwenye Elimu ya Ujasiriamali

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
1,915
Reaction score
3,422
Tokea mambo ya ujasiriamali yameanza kupamba moto hapa Tanzania, kumekuwa na upotoshwaji mkubwa sana ambao umekuwa unafanyika kwenye elimu ya ujasiriamali. Upotoshwaji huu umekuwa unafanywa na watu kwa kujua au wengine bila ya kujua, ila kwa kuwa unawanufaisha wao hawajali kuhusu wengine.
Kabla hata sijaenda mbali naomba niuseme upotoshaji wenyewe.
Ujasiriamali sio kutengeneza sabuni, wala sio kutengeneza mishumaa au kutengeneza mkaa wa makaratasi. Huu sio ujasiriamali na usikubali kuendelea kudanganywa tena.
Sisemi mafunzo haya ya kutengeneza vitu ni mabaya, hapana, ni mazuri sana. Ila ninachosema ni hiki; ukishajua kutengeneza sabuni haugeuki na kuwa mjasiriamali hapo hapo.
Ujuzi wa kutengeneza vitu mbalimbali mtu yeyote anaweza kujifunza, lakini sio kila anayejifunza anakuwa mjasiriamali, wengi wao wanafanya biashara zao kwa njia ambazo sio za kijasiriamali.
Ujasiriamali ni kabla na baada ya kutengeneza hiyo sabuni, lakini sio wakati unaitengeneza sabuni.
Kwa kukosa elimu sahihi ya ujasiriamali, watu wengi wamejifunza kutengeneza vitu mbalimbali ila hawajui soko liko wapi. Watu wanatengeneza sabuni zao vizuri na kuanza kuzunguka nazo, wanakosa wateja na mwishowe wanakata tamaa.
Leo nataka nikutambulishe kwa ufupi sana maana halisi ya ujasiriamali na elimu sahihi ya ujasiriamali unayotakiwa kuipata.

SOMA; Je Wewe Ni Mjasiriamali Au Mfanyabiashara Mdogo? Soma Hapa Kujua.

Nini maana ya ujasiriamali?
Ujasiriamali unajumuisha ubunifu, kutengeneza kitu kipya na kuwa tayari kukabiliana na ugumu; vilevile kuwa na uwezo wa kupanga na kuendeleza miradi ili kufikia malengo.
Ujasiriamali ni mtazamo katika akili ya mtu katika kutafuta fursa, kuwa tayari kukabiliana na matatizo na kuwa na uwezo wa kutengeneza faida, kwa kuanzisha ama biashara mpya au kuongeza tija katika taasisi.
Ujasiriamali hujumuisha shughuli nyingi ikiwa ni pamoja na kuwa na wazo, kutengeneza na kuendesha biashara.

Mjasiriamali ni mtu gani?
Mjasiriamali ni mtu anayefikiri kwa ubunifu na uvumbuzi akiwa tayari kukabiliana na hatari inayoweza kusababishwa na fursa zilizopo kwa lengo la kuzalisha faida, ajira na ustawi wa kijamii na kiuchumi.
Wajasiriamali huanzisha kampuni ambazo huwa injini katika ukuaji wa uchumi na utengenezaji wa utajiri. Kompyuta, simu za mkononi, mashine za kufulia, na huduma za usafirishaji ni mifano wa mawazo ya ujasiriamali yaliyobadilishwa kuwa bidhaa au huduma.
Kwa maana hiyo ya ujasiriamali na mjasiriamali tunaona kabisa kutengeneza sabuni ni sehemu ndogo sana ya ujasiriamali, kama hata ipo.

SOMA; Unapokuwa Tayari Kuingia Kwenye Ujasiriamali Fanya Vitu Hivi Vitano.

Elimu sahihi ya Ujasiriamali Unayotakiwa Kuipata.
Wewe kama mjasiriamali au kama ndio unataka kuingia kwenye ujasiriamali unatakiwa kupata elimu sahihi ya ujasiriamali. Elimu unayotakiwa kupata ni elimu ya kukubadili mtazamo, uache kuwa mtu wa kukata tamaa na kuogopa kujaribu na uweze kujaribu mambo mbalimbali. Pia elimu hii inatakiwa kukuandaa wewe uweze kutumia mazingira yako, vipaji vyako na matatizo ya watu wanaokuzunguka kuweza kuja na wazo ambalo litawanufaisha wote.
Kwa mfano kwenye kutengeneza sabuni kama tulivyotaja hapo juu, tumesema ujasiriamali ni kabla ya kutengeneza sabuni na baada ya kutengeneza sabuni.
Kabla ya kutengeneza sabuni kwanza unahitaji kujiuliza je kuna uhitaji wa sabuni? Kama ukitengeneza sabuni yako, nani atainunua? Mtu huyo anapatikana wapi na utamfikiaje? Na je mtu huyu ana uwezo kiasi gani wa kuweza kulipia sabuni unayotaka kuitengeneza? Na je gharama za kumfikia ni kiasi gani? Kwa kifupi unahitaji kuwa na mteja au kuweza kutengeneza mteja utakayeweza kumuuzia bidhaa au huduma unayotoa. Kama hujafikiria mteja wako ni mtu mwenye sifa gani, wewe sio mjasiriamali.
Baada ya kutengeneza sabuni yako pia kuna mambo muhimu ya kufanya. Kwa mfano tayari sabuni unayo ila mteja uliyemlenga hapatikani au hayupo tayari kununua, je unafanya nini? Au unakutana na ushindani mkubwa kwenye soko, au biashara inakuwa ngumu sana kiasi cha wewe kuingia kwenye hasara. Je unabadilishaje hali ya mambo? Hapa ndipo mjasiriamali wa kweli anapojulikana.

SOMA; Weka Pamoja Vitu Hivi Vitatu Na Tayari Wewe Ni Mjasiriamali Mwenye Mafanikio Makubwa.

Kwa kifupi elimu ya ujasiriamali ni elimu endelevu, ni elimu ambayo inatakiwa kufanyika kila siku. Yaani kama unataka kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio, hakikisha kila siku unapata nafasi ya kujifunza kitu muhimu. Jifunze kuhusu biashara, kuhusu maisha, kuhusu mafanikio, kuhusu kujiamini, kuhusu ubunifu na mengine mengi.
Uzuri ni kwamba tunaishi kwenye dunia ambayo kujifunza ni rahisi sana. Unaweza kujifunz akw akujisomea vitabu, kusoma mtandao wa intaneti, kuhudhuria semina, kujiandikisha kwenye kozi mbalimbali na hata kujifunza kupitia uzoefu na makosa unayoyafanya.
Moja ya maeneo muhimu ambapo utapata elimu kila siku itakayokubadili mtazamo wako na kukufanya kuwa mjasiriamali bora ni KISIMA CHA MAARIFA. Kwa kujiunga na KISIMA, unakuwa kwenye mazingira ambayo kila siku yanakupatia kitu kipya cha kujifunza kuhusu mafanikio kwenye kile unachofanya na maisha kwa ujumla. Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi.
Nafasi moja ya kukutana na mjasiriamali mwenye changamoto.
Natoa nafasi moja ya kukutana na mjasiriamali mwenye changamoto nyingi sana kwenye kile anachofanya na anaona anaelekea kukata tamaa. Kama unataka nafasi hii andika ujumbe mfupi kwenda 0717396253 kupata maelezo zaidi.
Unapokuwamjasiriamali, elimu yako ndio kwanza imeanza na usifikiri kuna siku utaacha kujifunza. Kama umeamua kweli kuingia kwenye ujasiriamali na unataka ufanikiwe kupitia ujasiriamali basi unahitaji kupata elimu sahihi kila siku ambayo itakufanya uendelee kuwa bora kila siku.
Nakutakia kila la kheri kwenye mafanikio kupitia ujasiriamali.
TUPO PAMOJA.
 
NAKUBALIANA NAWE, pia Ujasiliamali mzuri unatoka ndani ya mtu...mafunzo ya ujasiliamali huboresha zaidi hulka ya ujasiliamali. Si kila mtu anaweza kuwa mjasiliamali, ila aweza kuwa mfanya biashara. Ujasiliamali ni zaidi ya ufanyabiashara. Wengi wanachanganya haya maneno.
Mjasiliamali hawezi soma/jifunza huo unaitwa ujasiliamali kwanza ndio awe mjasiliamali....bali anazaliwa na hii hali (angalia maana ya ujasiliamali hapo kwa mleta mada)...Kisha akiongeza mafunzo yanayo tolewa na baadhi ya taasisi au watu binafsi HUONGEZA chachu ya mafanikio ya ujasiliamali wake....ningeshauri mafunzo ya ujasiliamali yanayotolewa na wengi kwa mjibu wa mtoa mada, yaitwe mafunzo ya biashara.
 
Asante Makirita kwa kuwafungua macho watu kuhusu ujasiriamali
 
Kuna wanaojiita wajasiriamali na kutoa mafunzo ya ujasiriamali. Ila mafunzo yao ni ya kinadharia mno, na hawajawahi kufanya mradi wowote unaoweza kuwa wa mfano.

Bwana Amani, wewe una mradi wowote?
Nini unaweza kutuambia tuyaamini mafunzo unayotoa?
 
Ujasirimali haufundishwi kinacho fundishwa ni Business skills, je unaweza fundisha mtu kuwa Commited? kuwa risk taker? kuwa inovative?
 
Lengo la makala hii sio kuibua mabishano kama ujasiriamali unaweza kufundishwa au la. Au tuje tuanze ubishani kama mjasiriamali anatengenezwa au anazaliwa.
Tuachane na hayo na tuangalie tunasaidianaje kama wajasiriamali ili tuweze kufanikiwa zaidi.
Kwa uzoefu wangu kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wengi wa kitanzania wanafanya mambo kimazoea sana. Na hii inawaumiza bila ya wao wenyewe kujua.
Ndio maana mimi nimejitoa kuzungumzia baadhi ya changamoto zinazowazuia wajasiriamali na wafanyabiashara wa kitanzania kufikia mafanikio wanayoweza kufikia.
Mfano watu wengi wana mtizamo hasi sana juu ya watu waliofanikiwa kwenye biashara, badala ya kuangalia wamefanya nini ili nao waige, wanakimbilia kusema wameiba, wamedhulumu, wamependelewa na kadhalika.
Watu wengi hawana mfumo mzuri wa kufuatilia mapato na matumizi yao. Mambo yanapokwenda vibaya wanaanza kulaumu mara chuma ulete mara kizizi na kadhalika.
Watu wengi wanajiingiza kwenye ujasiriamali/biashara kwa kuiga kitu ambacho kinawafanya wajikute kwenye ushindani mkubwa sana unaopelekea biashara zao kufa.
Haya ndio mambo ambayo mimi nayafanyia kazi, na kuwashirikisha wale ambao watapenda kujifunza na kuyatumia kwenye biashara zao.
Ila kwa atakayetaka tu kubishana, sitakuwa na muda huo.
TUPO PAMOJA.
 
mi nitakuwa tofauti na wewe pia naweza kukuunga mkono,Elimu ya ujasiriamali bila mafunzo ni kazi bure watu wamechoka na mmaneno tu matupu mwisho wa siku hawajui wafanye nini.

Ambacho ni sahihi pamoja na kupatiwa elimu ya ujasiriamali lazima wajue mafunzo ya vitendo yatakayowasaidia maneno tu hayatoshi,mkimsikiliza mtoa mada inakula kwenu,nyie endeleeni kupata mafunzo mbalimbali yatakayowasaidia kufanya shuguli kwa vitendo lakin mkiwa mnasikiliza maneno tu mwisho wa siku hamjui mfanye nini

Hili jambo ndio linalotokea ata kwenye elimu yetu profesa anajua kufundisha tu kwa vitendo hakuna kitu hajui ata kitu cha kufanya,siku hakistafu anakufa ghafla kwa presha kwa mawazo.

Nyie endeleeni kupata ujasiriamali kwa vitendo mtafaidika na maisha lakin bila hivyo,mtoa mada kula yake ni kufundisha ujasiriamali lakin hana mradi wowote .

ni hayo tu
 
Nashukuru Amakirita Umenisaidia Nakukumbuka Tulisoma Wote Shule Moja 'O' Level Pale Dodoma Bila Shaka Wewe Ni Some Body 'ngwangwalu',kwa Wanaohitaji Mafunzo Haya Tafuta Post Yangu Inayokwenda Kwa Jina 'NATOA MAFUNZO YA KUTENGENEZA BIDHAA MBALIMBALI', Karibuni wote
 
Back
Top Bottom