Tukiwa tumebakiwa na wiki tatu tu Watanzania tupige kura kuchagua Rais, wabunge na madiwani.
Licha ya kuwa na wagombea 15 wa kiti cha Rais lakini mpaka sasa wenye nguvu ya ushawishi ni kutoka vyama viwili vya CCM na CHADEMA.
Lakini kumekuwepo na kutumia nguvu kubwa sana kujaribu kupotosha kauli ya mgombea wa CHADEMA kwenye kampeni zake.
Wapinzani wake mara nyingi wamekuwa wakipotosha kwamba anasema kwenye uchaguzi huu lazima yeye atangazwe mshindi na kwamba asipotangazwa basi ataingiza watu barabarani.
Wenye kueneza upotoshaji huu kwangu mimi nawafananisha na maadui wa taifa hili kwasababu wanajaribu kumjengea chuki ya makusudi Mh.Lissu ili aonekane yeye yupo kwa ajili ya kuleta vurugu.
Lakini haishangazi maana watu hao hao ndio wanasema Lissu ametumwa na Mabeberu, mara akishinda atauza nchi.
Hawa ni wapotoshaji ambao kwa kiasi kikubwa wametawaliwa na ubinafsi, unafiki, na uchu wa kutawala ambao lengo lake si kwa maslahi mapana ya nchi na wananchi wote bali wao na familia zao.
Lissu mara zote ameweka wazi msimamo wake kwamba pamoja na tume kutokuwa huru lakini anachotaka ni uchaguzi wa haki na huru. Kwa maana kwamba kusiwepo na mizengwe na figisu figisu kama ilivyozoeleka kwenye chaguzi zote. Amesema akishindwa kwa haki hatakuwa na shida na yeyote na atakuwa wa kwanza kukubali matokeo, kinyume chake anesema hakitaeleweka.
Sasa unajiuliza hawa wapotoshaji wanaogopa nini kuendesha uchaguzi wa huru haki na uwazi? Kama wanaamini wanakubalika sana kwa watanzania kwa namna wanavyoongoza nchi sasa hofu yao inatokana na nini?
Ukijaribu kuitafakari kauli yao kwamba Lissu ametumwa na Mabeberu na kwamba akishinda urais atauza nchi, yaani utagundua kuwa ni kauli ya kipuuzi iliyokosa maana kabisa.
Maana Lissu ni mtanzania kama walivyo wao, tofauti yao ni kwamba wakati Lissu amepambana kwa miaka 17 kutetea raslimali za nchi hii, hao wapotoshaji walikuwepo na hawajawahi kukemea au kusema lolote juu ya ujambazi unaofanyika kwenye raslimali asili zetu kwa baraka za ccm. Zaidi sana wakamuona Lissu kama anakwamisha maendeleo wakamfungulia kesi ili wafunge.
Lissu kwa miaka yote ameonekana kuwa adui mkubwa wa serikali ya CCM kwasababu ya msimamo wake wa kutetea raslimali za nchi hii. Mpaka sasa raslimali zetu zinaendelea kuwafaidisha hao wanaoitwa mabeberu kama walivyokabidhiwa na serikali ya ccm kupitia sera waliyoibatiza jina la wawekezaji..
Wapotoshaji hao hapo huwezi kuwasikia wakisema lolote.
Watanzania tuamke usingizini, hawa wenzetu wanachokipigania ni maslahi yao na ya familia zao. Wanaona ujio wa Lissu ni tishio kwao na kwamba akishinda hivyo madhambi yao yatawekwa wazi ndio maana wanapigana kufa na kupona kumzuia asishinde ili kulinda madhambi yao.
Mtazania shtuka.