Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,972
1. Zimekuwa zikitolewa kauli mara kwa mara kwamba kuna watu wasiowatakia mema waislamu kiasi kwamba hawataki wawe na Mahakama za Kadhi ambazo ni sehemu ya Ibada zao! Kauli hizo zimekuwa zikipotosha ukweli ama kwa makusudi au kwa kutokujua juu ya jambo hilo.
2. Mara kwa mara linapotokea suala la Kadhi utasikia suala la Ubalozi wa Vatican likijitokeza kama vile Ubalozi huo unagharimiwa na Serikali ya Tanzania. Hata hivyo suala la Balozi nyingine ambazo nchi zao au Serikali zao ni za Kidini halizungumzwi kabisa, it is a one sided story!
3. Suala kubwa toka kwa watu wasio Waislamu ni kwamba Mahakama hizo ziruhusiwe, kwa kuwa ni haki kwa Waislamu kuwa nazo, hata hivyo sijui kama wameangalia kwa marefu na mapana juu ya mahakama hizo!
(a) Tumesikia kwamba Mahakama za Kadhi zitahusu Ndoa, Talaka na Mirathi tu. Ukiangalia kwa haraka haraka ni kama vitu vyenyewe si vizito sana kuingizwa kwenye Sheria zetu za kawaida na kushughulikiwa na Majaji wetu kama zilivyoingizwa Sheria nyinginezo. Hata hivyo katika kuonesha kwamba hii ni sehemu ya Ibada ya Kiislamu hawataki suala hili kushughulikiwa na watu wasiokuwa Waislamu! Kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba waislamu wanataka kufanya mambo yao bila kuingiliwa na Serikali.
(b) Hata hivyo, inavyoonekana mambo sivyo yalivyo. Ukiangalia Mahakama za Kadhi kwa Zanzibar, Chief Kadhi huteuliwa na Rais wa Zanzibar. Kwa Zanzibar sina neno sana kwa kuwa 99% ya Wazanzibari ni Waislamu, kwa hiyo probability ya kuwa na Rais mwislamu ni kubwa. Hata hivyo akitokea Rais ambaye ni Mkristo itabidi amteue huyo CK bila kupenda!
(c) Kwa upande wa uendeshaji wa Mahakama hizo kwa upande wa gharama, Waislamu wanataka Serikali ndiyo igharamie Mahakama hizo! Hapo ndio matatizo yanapoanzia! Kama nilivyosema kwamba Mambo ya Mahakama za Kadhi ni Ibada ya Waislamu. Ibara ya 19 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inasema kwamba "Kazi ya kutangaza dini, kufanya Ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi." Kwa hiyo Serikali itakapotia mguu kugharamia Mahakama za Kadhi itakuwa imejiingiza kutangaza dini ya Kiislamu ambapo itakuwa ni kuvunja Katiba!
(d) Pamoja na kwamba Mahakama za Kadhi zitajihusisha na ndoa kama nilivyosema hapo mwanzo, suala la ndoa ni pana. Ndio maana tumeona kwamba kuna Sheria za Kiislamu za KUPIGA WATU MAWE hadi kufa kwa kosa la uzinzi! Yapo pia makosa ambayo yanasema kwamba ni kosa kwa wanaume kuchanganyika na wanawake (haya yapo kwenye nchi za kiislamu, lakini msingi wake ndio huo). Suala la kujiuliza ni kwamba kama Mahakama za Kadhi zinaweza kuachiwa BAADHI YA MAMBO tu na mengine kushughulikiwa na Serikali (eg adhabu za kupiga mawe zisiwepo), Je, Mahakama hizo kwa nini ziwepo? Wasio Waislamu wanaona kwamba haya mambo ya Mahakama ya Kadhi ni NJIA YA KUISILIMISHA nchi baadaye!
4. Wasio Waislamu wanachotaka ni kwamba Waislamu waachiwe mambo yao wenyewe na Serikali isijiingize kwa namna yoyote ile katika kumteua Kadhi Mkuu (KM) au kuyagharamia!
5. Nchi za Nigeria, Somalia, Sudan na nyinginezo zimeingia katika migogoro ya kidini na hata kufikiria kuzigawanya baadhi ya nchi hizo ili Wakristo wakae peke yao, pia Waislamu wawe hivyo hivyo peke yao. Mauaji yasiyokoma, uchomaji Misikiti na Makanisa umetokea ili mradi tu kuonesha hasira walizonazo baadhi ya watu wa dini moja dhidi ya dini nyingine.
6. Zipo hoja ambazo zimetolewa kwamba baadhi ya nchi zina Mahakama za Kadhi lakini hakuna fujo za aina yoyote! Kwa mwenye macho ya kutazama na masikio ya kusikia hawezi kubishana na mimi kwamba kama Serikali itaamua kuibeba dini moja kwa maslahi ya dini hiyo tunao mgogoro mkubwa wa kidini katika siku za mbeleni, kwa sababu dalili zote zipo. Kila iitwapo leo amani ya nchi yetu inazidi kutoweka taratibu! Tutazame nchi yetu mambo yanavyokwenda badala ya ku-copy n' paste mambo ya nchi nyingine! Tukilazimisha mambo tutakuja kulia siku moja na hakuna pa kukimbilia maana kwa majirani zetu si wakarimu kama sisi, wanachukia mno wageni!
7. Amani yetu ni kama barafu, tusiiruhusu ikaanza kupigwa na jua itaanza kuyeyuka taratibu na mwisho wa siku tutakuwa na maji ya moto badala ya barafu!
8. Wasio Waislamu wanawatakia mema Waislamu, ndio maana wanataka Waislamu washughulikie mambo yao ya kiibada bila kuingiliwa na Serikali kiuendeshaji au kwa gharama kwa manufaa yao na bila kuvunja Sheria za Nchi, ikiwemo Sheria mama, Katiba!
Naomba kuwasilisha, kwa mjadala zaidi, kama upo!