Upumuaji (ventilation)

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Unapolala sehemu kubwa ya mwili inakuwa imepumzika, viungo vinavyoendelea kufanya kazi katika mwili ni moyo, diaphragm na macho pamoja na kuwa yanakuwa yamefumbwa. Mwili unahitaji oxygen ili ufanye kazi na unatoa carbon dioxide kama uchafu wa chembe hai za mwili.

Njia kuu ya kubadilisha hewa hizo mbili za muhimu ni kwa njia ya kupumua. Kwa wale wenye matatizo ya mapafu kama, pumu sugu, chronic obstructive pulmonary diseases (COPD) na unene kupitiliza (obesity) uwezo wao wa kupumua unakuwa umepungua au unahitilafu. Hii inamaana kuwa unapolala uwezo wa mwili kutoa carbon dioxide unapungua. Kawaida carbon dioxide inatoka mwilini kwa njia mbili ku exhale (kutoa pumzi) na farting (kujamba).

Carbon dioxide inapokuwa nyingi mwilini, mwili unapoteza pH balance na damu inakuwa katika hali ya acidic (acidosis). Hali hii humfanya mtu kuamka akiwa na maumivu ya kichwa, kuchoka, kusikia kizunguzungu. Mara nyingi watu wanasema nikiamka lazima nipate paracetamol au Panadol ndiyo nitoke kitandani.

Inachotokea hapa ni kuwa, kwasababu ukiamka viungo vya mwili vinaendelea kufanya kazi kama kawaida, breathing muscles na nerves zinasaidia kutoa carbon dioxide mwilini, na baada ya muda unajisikia kichwa kimeacha kuuma na pia kizunguzungu kimeacha. Unachotakiwa kufanya hapa, ni kukaa kidogo kitandani kama unasikia kizunguzungu, pumua kwa dakika chache, kama unaweza kuvaa na kutoka kutembea kwenye garden (kama inawezekana) kutakupa fresh air na kubalance pH levels.

Kama ni tatizo sugu ni kheri kwenda hospitali ambako utachekiwa Arterial Blood Gas (ABG).
 
Hii elimu nzuri saana...
N mmoja wa wahanga wa hali io
 
Yaah..
Kuumwa kichwa morning then knakata u nakula hdex
Jaribu kufanya hayo hapo juu utagundua kuwa huhitaji hdex. Pia ni muhimu kuchekiwa ABG ili wajue pH na acid levels kwenye damu.
 
Jaribu kufanya hayo hapo juu utagundua kuwa huhitaji hdex. Pia ni muhimu kuchekiwa ABG ili wajue pH na acid levels kwenye damu.
Shukran mkuu,sema sorry ABG n nn
 
Nahitaji mke daktari
Mwenye MD
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…