#COVID19 Upungufu wa Chanjo wapelekea Serikali ya Namibia kusitisha utoaji wa dozi ya pili

#COVID19 Upungufu wa Chanjo wapelekea Serikali ya Namibia kusitisha utoaji wa dozi ya pili

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Nchi hiyo imeacha kutoa Dozi ya pili ya Chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19 ili kutoa kipaumbele kwa wale ambao bado hawajapata Dozi ya kwanza.

Kutokana na upungufu, Serikali imesema itagawa Chanjo zilizobaki katika maeneo ambayo yameripoti ongezeko la maambukizi na vifo, na ambao wanasubiri Dozi ya pili watasubiri hadi Julai.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Taifa hilo, Dozi za AstraZeneca zinatarajiwa kuwasili mwezi Julai kupitia Mpango wa COVAX.

=====

Namibia has stopped giving second Covid-19 vaccine doses to prioritise those who are yet to receive their first jabs as supplies dwindle

The health ministry said it will redistribute its remaining Covid-19 vaccine stock to areas with increased virus cases and fatalities

The ministry said those due for their second dose will only be vaccinated in July when new stocks arrive

The Namibian news site reported that the country had run out of the China-made Sinopharm vaccine

The health ministry said it was expecting AstraZeneca doses in July through the Covax scheme.

Source: BBC
 
Waafrica hembu tuacheni ujinga, kuliko kuwa covax si ni bora kama nchi itoe hela inunuwe tu chanjo za kutosha? Ya nini kuombaomba wakati hela zipo? Hivi ni kweli nchi kama nchi inakosa hela ya kununua chanjo?maisha ya raia ni priceless wajameni
 
Hili suala la dozi halihitaji ubabaishaji kabisa. Ukiamua kutoa chanjo inabidi uwe nazo za kutosha kukamilisha dozi.

Kwa mfano, dozi ni sindano tatu, kila mwezi sindano moja. Je, itakuwaje kama chanjo zinaisha halafu mtu ameishia sindano ya pili, na chanjo zinakuja baada ya miezi minne? Je, itabidi aanze upya au aendelee? na akiendelea itakuwa inafanya kazi?
 
Back
Top Bottom