Dr isaya febu
Member
- Jan 17, 2023
- 40
- 294
Upungufu wa damu kwa mjamzito ni hali inayotokea wakati kiwango cha hemoglobini katika damu kinapungua chini ya kiwango kinachohitajika (<11 g/dl), hasa wakati wa ujauzito. Hemoglobini ni protini inayopatikana kwenye seli nyekundu za damu na inasaidia kusafirisha oksijeni mwilini., hivyo upungufu wake unaweza kuathiri afya ya mama na mtoto.
Upungufu wa damu kwa mjamzito hujulikana kwa kitaalamu kama anaemia in pregnancy.
Aina hii ya upungufu wa damu unaosababishwa na upungufu wa madini ya chuma wakati wa ujauzito hujulikana kwa kitaalamu kama iron deficiency anaemia.
Ukosefu wa foliki asidi wakati wa ujauzito unaweza kusababisha upungufu wa damu na kuongeza hatari ya matatizo kwa mtoto, kama vile kasoro za mfumo wa neva (neural tube defects).
Aina hii ya upungufu wa damu unaosababishwa na upungufu wa foliki asidi wakati wa ujauzito hujulikana kwa kitaalamu kama folic acid deficiency anaemia.
Lishe isiyo na vyanzo vya vitamini B12 kama vile maziwa, mayai, samaki, na nyama inaweza kusababisha upungufu wa damu wakati wa ujauzito.
Aina hii ya upungufu wa damu unaosababishwa na upungufu wa vitamini B12 wakati wa ujauzito hujulikana kwa kitaalamu kama vitamin B12 deficiency anaemia.
1) Uchovu wa mara kwa mara (easy fatigability)
2) Kizunguzungu (dizziness)
3) Mapigo ya moyo kwenda kasi (heart palpitation)
4) Kupumua kwa shida (shortness of breath)
5) Ngozi, midomo (lips), na kucha kuwa na rangi iliyopauka (paleness)
Upungufu wa damu kwa mjamzito hujulikana kwa kitaalamu kama anaemia in pregnancy.
Sababu Kuu Za Upungufu Wa Damu Kwa Mjamzito:
Zifuatazo ni sababu kuu zinazochangia upungufu wa damu kwa mjamzito:1) Upungufu Wa Madini Ya Chuma.
Wakati wa ujauzito, uhitaji ya madini ya chuma huongezeka ili kusaidia katika utengenezaji wa seli nyekundu za damu mpya kwa ajili ya mama na mtoto aliye tumboni. Hivyo basi, lishe duni, ufyonzwaji duni wa madini ya chuma mwilini, au mahitaji makubwa ya madini ya chuma wakati wa ujauzito husababisha upungufu wa damu.Aina hii ya upungufu wa damu unaosababishwa na upungufu wa madini ya chuma wakati wa ujauzito hujulikana kwa kitaalamu kama iron deficiency anaemia.
2) Upungufu Wa Foliki Asidi (Vitamini B9).
Foliki asidi (vitamini B9) inahitajika kwa utengenezaji wa seli nyekundu za damu.Ukosefu wa foliki asidi wakati wa ujauzito unaweza kusababisha upungufu wa damu na kuongeza hatari ya matatizo kwa mtoto, kama vile kasoro za mfumo wa neva (neural tube defects).
Aina hii ya upungufu wa damu unaosababishwa na upungufu wa foliki asidi wakati wa ujauzito hujulikana kwa kitaalamu kama folic acid deficiency anaemia.
3) Upungufu Wa Vitamini B12.
Vitamini B12 ni muhimu kwa utengenezaji wa damu na mfumo wa neva wa mtoto.Lishe isiyo na vyanzo vya vitamini B12 kama vile maziwa, mayai, samaki, na nyama inaweza kusababisha upungufu wa damu wakati wa ujauzito.
Aina hii ya upungufu wa damu unaosababishwa na upungufu wa vitamini B12 wakati wa ujauzito hujulikana kwa kitaalamu kama vitamin B12 deficiency anaemia.
4) Magonjwa Na Maambukizi.
Magonjwa kama vile malaria, minyoo tumboni, na magonjwa sugu yanayoathiri utengenezaji wa seli nyekundu za damu yanaweza kusababisha upungufu wa damu kwa mjamzito.5) Kupoteza Damu Kwa Kiasi Kikubwa.
Kutokwa na damu nyingi kabla au wakati wa ujauzito, kama vile kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi kabla ya mimba, huweza kusababisha upungufu wa damu.Dalili Za Upungufu Wa Damu Kwa Mjamzito:
Dalili zinaweza kuwa tofauti kulingana na kiwango cha upungufu wa damu. Dalili za kawaida ni pamoja na:1) Uchovu wa mara kwa mara (easy fatigability)
2) Kizunguzungu (dizziness)
3) Mapigo ya moyo kwenda kasi (heart palpitation)
4) Kupumua kwa shida (shortness of breath)
5) Ngozi, midomo (lips), na kucha kuwa na rangi iliyopauka (paleness)