Ngufumu
Member
- Dec 29, 2016
- 25
- 44
Je Unaijua Homoni ya Kiume/Testestrone?
Leo tuzungumze kidogo kuhusu Homoni ya Kiume/ Testestrone. Kwani upungufu wa hivi vichocheo huweza kuleta madhara makubwa sana siyo tu kitandani bali hata kwenye maisha ya kawaida ya mwanaume hata Mwanamke pia, lakini usjali suluhu ipo
Disclaimer: Ujumbe huu ni kwa lengo la kuhabarisha tu na si vinginevyo, usitumike kama njia ya matibabu, kinga wala ushauri wa kiafya. Kwa taarifa sahihi za kiafya wasiliana na Daktari wako au mtaalamu mwenye Leseni ya kutoa huduma za Afya au fika kituo cha kutolea huduma za afya kwa matibabu stahiki. Ukiwa na dharura ya kiafya piga simu namba 199 kutoa taarifa na kuitisha msaada.
Testestrone
Ni homoni kuu ya jinsia ya kiume na inahusika na maendeleo, mabadiliko na sifa nyingi za kimwili zinazotambulika kama sifa za kiume/ sifa za mwanaume halisi kama vile Sauti nzito, ukuaji wa nywele usoni, sehemu za siri na maeneo mengine ya mwili, kuongezeka kwa uzito na ujazo wa mifupa(bony density), na zingine nyingi.
Testosterone, ni sehemu ya kundi la homoni linajulikana kama androjeni, hutolewa na tezi dume baada ya msisimko kutoka kwa tezi ya pituitari, ambayo iko karibu na sehemu ya chini ya ubongo na ishara hutumwa kwa korodani za kiume ambazo huamsha hisia za hamu ya tendo la ndoa, Ingawa testosterone inaweza kutumika kutibu wanawake(wanayo pia lakn kwa kiasi kidogo), viwango vya chini vya testosterone (au hypogonadism) huchukuliwa kuwa tatizo la wanaume.
Dalili za upungufu wa Homoni ya Kiume
=> Dalili kwa vijana Wadogo/vijana balehe
1. Kuchelewa kubalehe
2. Kukosa tabia za ukuaji wa kijinsia kama vile Sauti nzito na minywele usoni
3. Maumbile madogo ya via vya uzazi
=> Dalili kwa vijana wa rika la kati na wakongwe
1. Uchovu
2. Kukosa hamu ya tendo
3. Msongo wa mawazo
4. Kukosa usingizi/ matatizo ya usingizi
5. Kukosa uwezo wa Kusimamisha/ kudindisha au kusimamisha kilegelege
6. Kuwa na mbegu chache za kiume(Mpaka vipimo vya maabara vithibitishe)
7. Kupoteza misuli na mifupa dhaifu/mepesi( uzito mdogo/ ukondefu)
8. Matatizo ya uzazi
9. Kupoteza nywele, siyo kipara😁
Nb: Baadhi ya dalili kama uchovu uchovu, kukosa usingizi, msongo wa mawazo n.k zinaweza kuwa zimetokana na maradhi mengine na zisiwe na uhusiano wowote na tatizo hili. Pia Siyo wote wenye upungufu wa Homoni hii wataonyesha dalili.
=>Sababu na Vichocheo vinavyo pelekea tatizo la upungufu wa Homoni ya Kiume/Testestrone
1. Kikawaida Homoni hizi huanza kupungua kwanzia kwenye umri wa miaka 30 kwa 1% kila mwaka kadiri miaka inavyosonga
2. Matatizo ya kiafya kama vile Tatizo la kinga mwili kushambuliana zenyewe kwa zenyewe, matatizo ya Kijenetiki, Matatizo ya Figo, matatizo ya Mapafu, UKIMWI, matatizo ya moyo, Maambukizi kama vile matumbwitumbwi(Mumps), Ajali/ majereha ya Korodani, Unene kupitiliza, Kisukari na Kansa ya Korodani kati ya mengi
3. Matumizi ya baadhi ya dawa na Kemikali kama vile Matumizi ya Pombe, Dawa za kansa za kemikali(Chemotherapy), dawa aina ya steroids zinazotumika kupunguza uvimbe au kwenye pumu na matumizi dawa zilizopo ktk kundi la Opioids kutuliza maumivu, kama madawa ya kulevya au kutibu uteja/uraibu madawa kama Morphine, Fentanyl, Methadone na Cocaine
4. Sababu zingine zinazosababisha upungufu wa Homoni hii kwa mwanaume hazijulikani yaani inatokea tu. Na wengi wenye upungufu huo umesababishwa na sababu zaidi ya moja.
=> Uchunguzi na Matibabu
Zipo Njia za kitaalamu za uchunguzi wa tatizo hili ambazo zinahusisha vipimo mbalimbali vya maabara. Pia zipo tiba mbalimbali za kitaalamu kabisa moja wapo ni Testestrone Replacement Therapy (TRT- japo inapendekezwa utumiwe na wenye upungufu wa nguvu za kiume/ sexual dysfunction tu) hizi hatutoziongelea zaidi ya hapo
=>Tuzungumze namna ya kujikinga na Tatizo hili kwa njia za kawaida kabisa
1. Lishe
Hapa ndipo pakuzingatiwa zaidi na wanaume wengi, Ulaji unaotakiwa ni ulaji unaozingatia mlo kamili lakini pia kupunguza ulaji wa mafuta hatari(bad cholesterol) badala yake kula vyakula vya mafuta safi kama vile karanga, parachichi na Mzeituni/olive oil, epuka matumizi ya vinywaji na vyakula vya Makopo hasa ya plastiki yana kemikali aina ya Bisphenol A(BPA) inayopunguza Homoni hii
Zingatia ulaji wa Madini ya Zinki kila siku kwani hayaifaziwi mwilini na yanahitajika kwa kiasi kikubwa(12mg - 15mg kwa siku) kwa mwanaume, yanapatikana kwenye samaki aina ya shellfish 🦐 kama vile chaza au kaa 🦀, mbegu za maboga, Nguruwe n.k pia punguza matumizi ya Sukari sana inapunguza hii homoni.
2. Badili mtindo wa maisha
Acha tabia ya unywaji wa pombe kwani kama tulivyoona pombe ni sababu ya Upungufu wa homoni hii muhimu kwa uanaume wa mwanaume
Punguza uzito uendane na urefu wako kwani uzito kupindukia nao ni chanzo cha tatizo hili, tumia formula ya Prof. Janabi chukua urefu wako kwa sentimita toa mia moja kinachobaki ndio uzito wako unatakiwa kucheza hapo. Watafute wataalamu wa kupunguza uzito wakusaidie
Fanya mazoezi jenga misuli ambayo itasaidia Testestrone itolewe kutoka kwenye protein iliyohifadhiwa katika mfumo wa misuli, punguza mafuta/kitambi jenga misuli, iwe mwisho kuwakejeli waenda gym🤗
3. Punguza mawazo
Kama tulivyoona msongo wa mawazo ni sababu ya homoni hii kupungua jenga tabia ya kuzungumza na watu unao waamini juu ya changamoto zako usiache stress zikageuka msongo wa mawazo itakugharimu. Homoni ya stress “Cortisol” inaweza ikapunguza ufanisi wa Testestrone
4. Pata usingizi wa kutosha
Punguza matumizi ya mwanga wa simu, kompyuta na Tv usiku ili uweze kulala, fanya kazi za kuchosha mwili mchana lala mapema masaa 8 kwa siku yakukute umepiga mboji.
Tutaendelea tukijaaliwa
Mimi ni Kaka Gift, nakusanua tu
Kuendelea kula nondo kama hizi save namba yangu👇🏾