Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,187
Iodine ni madini yanayozalishwa baharini na kumwagwa nchi kavu ambako yanaingia chini kwenye miamba, hivyo upatikanaji wake unategemea zaidi aina ya udongo na vyakula vya baharini. Kutokana na mmomonyoko wa udongo, ardhi inazidi kuishiwa na madini hayo. Aidha, kadri unavyoingia ndani (interior) kutoka baharini na pia kadri unavyopanda mwinuko (altitude) ndivyo IDD inavyoongezeka.
Iodine ni mojawapo ya madini muhimu kwa usitawi na ukuaji wa binadamu kwa kuwa ndiyo chakula lishe (micro-nutrients) pekee chenye athari kubwa katika maendeleo ya ubongo hasa katika hatua ya mimba (fetal brain development).
Duniani, watu bilioni moja wako kwenye risk ya kupata madhara kwenye ubongo kutokana na Iodine Deficiency Disorder (IDD) ambapo athari yake katika utambuzi (cognition) ndiyo chanzo kikuu cha utofauti wa ukuaji kati ya jamii na jamii.
Kiasili, 41% ya Watanzania in 1980s, sawa na watu milioni 10, waliishi maeneo yenye tatizo la IDD, ambalo 25% walikuwa na IDD huku 3% wakiwa na kiwango cha juu kabisa (severe). Aidha, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizokuwa na kiwango cha juu kabisa cha IDD duniani.
Katika baadhi ya maeneo ya Nyanda za Juu Kusini Total Goitre Prevalence (TGP) ilifikia 90% huku nusu ya watoto wakiwa na Tezi (hypothyroid). Maeneo hayo ni miongoni mwa Wilaya 27 zilizo-targetiwa kuanza kupewa iodised oil capsules. Wilaya hizo ni zifuatazo:
Soma baadhi ya maandiko yafuatayo:
In Raising the World’s I.Q., the Secret’s in the Salt
https://pdfs.semanticscholar.org/44...759.135366478.1525811663-689191352.1525811663