Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Wiki mbili mfululizo sasa kumekuwepo na kelele nyingi kila kona ya nchi kuhusu upungufu na mgao ya maji katika miji na majiji.
Katika maeneo ya vijijini sehemu nyingi za nchi maji limekuwa tatizo kubwa toka nchi hii inapata uhuru lakini hatujawahi kusikia kelele na mayowe kama wiki hizi mbili. Maji huko ni bidhaa adimu, ni aina fulani ya anasa. Wanawake, watoto kwa wanaume ni kawaida kabisa kutembea maili nyingi kufuata maji yasiyo safi wala salama kila siku wanayoishi chini ya jua.
Hizi kelele na yowe za wiki mbili zina tafsiri gani tofauti na ubinafsi mkuu kwa kuzingatia watu wengi wanaoishi mijini wametoka katika vijiji hivyo ila hawakuwahi kujihusisha na kupiga kelele kuchochea jitihada zozote za upatikanaji maji mpaka walipoguswa na kadhia hii?
Tanzania ni kubwa kuliko mtaa na kijiji chako, sote tunawajibika kuifanya nchi hii bora kwa kila mmoja anayeisha sasa na atakayekuja baadaye.