MAMA POROJO
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 4,974
- 785
hii serikali ya m''kwere ni vururuvururu tu tangu aingie madarakani, sasa wanaharibu hadi nature ya magogoni, uuuuuuwiiiiiiiiiiiiiii.....niikahi moyo wangu.
Kwa sasa taarifa hii haijitoshelezi ni kama inakosa maelezo ya zaida, aliyetuma thread hii ameshitushwa na design ya majengo bila kujali kwamba Ikulu inatakiwa kujengwa kwa kiwango cha hali ya juu kupita kiasi na ndio maana Ikulu kama ya USA iko karne nyingi kwa sababu waliwekeza kwa ajili ya kizazi kijacho.
Wewe mama mbona uko bize sana kujibu Inaonekana umetumwa nini? Hebu tuambie kama project hii ni priority kwa hali ngumu ya kifedha na ugumu maisha tulionao. Wananchi wengi hivi sasa tumesimamisha project zote za maendeleo na kubaki na kuganga njaa tu maana kipato hakitoshi kufanya Project yoyote ya maendeleo labda kama wewe ni fisadi.
Kaanei chini mfikiri kama project hii ni priority kwa sasa. Pia tungetamani kufahamu gharama ya hii project maana kama kawaida lazima itakuwa ni inflated value project kama kawaida ya mafisadi.
Nieleweshe mkuu labda kweli sijaelewa.
Ukumbi Ikulu? wenye majiko na VIP Rooms?.....Tumetishika zaidi na mchoro ambao sina hakika kama ndio wenyewe kweli na kuacha kujadili faida ya mradi huu. Wote tunakimbilia kwenye thamani ya ujenzi sio tutaokoa kiasi gani baada ya ujenzi huo kukamilika. Moja ya maeneo ambayo yanaingiza hasara serikali kwa sasa ni kukodi kumbi za kisasa kulingana na wakati uliopo huko nyumba serikali haikuwekeza kwenye kumbi. Kama kweli tunataka serikali yetu iache kukodi kumbi wakati wa mikutano ya ndani na kimataifa tunahitaji angalau kuanza kujenga ukumbi mmoja mmoja kadri miaka inavyosonga mbele
International conferences Ikulu? what next - kitchen party?
Ni Ikulu gani duniani inatumiwa kwa 'international conferences? Usalama utakuwaje?
Hivi tuna shida ya huo ukumbi?
Ina maana NSSF ndio wanajenga huuu ukumbi?Hii ni njia nyingine huyu mkweree na genge lake wamebuni mradi kutaka kwaibia masikini wananchi ; wakati wanasema hawana fedha za kulipa mishahara ya madaktari lakini wanazo fedha za majengo!! Hizo fedha za NSSF nyie jamani ni za wenyewe wafanyakazi msizimalize kwa maslahi yenu binafsi, kama mna shida ya ukumbi wa kimataifa mbona ule pale benki kuu umejengwa kwa mabiioni ya fedha na hautumiki!!