upuuzi wa pori la akiba la selous

upuuzi wa pori la akiba la selous

lerique

Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
21
Reaction score
2
habari wapendwa?
mimi ni kati ya watu ambao kimsingi nachukizwa sana na watu wachache ambao wanatumia maliasili kua sehemu za kujinufaisha wao na familia zao lakini wanasahau yakua watanzania walio wengi wanashindwa kua na maisha bora kwa sababu keki ya taifa inaliwa na mapanya haya.
mimi nataka kuzungumzia upuuzi (samahani kwa lugha hii) wa kiongozi wa mradi wa pori la akiba la selous bwana Benson Kibonde ambae amekua akifanya mradi huu kama ni wakwake na kibaya zaidi serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii idara ya wanyamapori imeamua kumpa mkataba wa miaka miwili wakati madudu anayoyafanya katika uhifadhi ni aibu.
kimsingi ni mchapakazi lakini conservation is multidiscplinary concepts ambazo kwa pamoja ndio uhifadhi unafanikiwa.Bwana huyu amekua akihodhi ofisi yeye mwenyewe kwa utashi wake.yani yeye anachojua uhifadhi is all about combating poaching na anasahau kabisa kwamba factors zipo nyingi zinazoweza kumaintain carrying capacity ya animals within their habitats kwa kuangalia ecology ya sehemu husika.
Pori la selous lina ukubwa wa kilometa za mraba zipatazo 50000 ambazo kwa ideology anayotumia ya anti poaching to me it is senseless maana kwa idadi ya askari waliopo katika pori hili lenye kanda 8 za Matambwe,Kingupira,Liwale,Kalulu,Seka(ambapo kuna machimbo ya URANIUM),Ilonga,Msolwa na Miguruwe.Kanda hizi zote zina jumla ya askari wapatao 2400,hivi kwa akili ya kawaida hapa unafanyaje doria kucover eneo la ukubwa wa kmsq50,000?
Kibande yawezekana anaonekana ni mchapakazi lakini hebu sikieni hili!Jatika kanda zote hakuna kanda zenye magari thabiti ya kufanyia doria na gari zote zikiharibika anataka zikatengenezwe dar es salaam ambapo kuna ofisi ndogo za selous pale ivory room wakati katika kila kanda kuna karakana kubwa na nzuri ambazo matengenezo yanaweza kufanyika.
Nilifurahshwa sana na makala ya Mh. Zitto Kabwe aliyoandika katika gazeti la Raia Mwema kuelezea ujangili uliokithiri katika pori hilo.Ametoa takwimu sahihi kabisa ambaxo kimsingi najua zimewakera walaji lakini AMINI MSIAMINI HALI NO MBAYA KATIKA PORI LA SELOUS ingawa watumishi wanajituma sana kufanya kazi lakini mkuu huyu amekua mbabe na asiesikia kitu.
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, sasa umefika wakati kwa serikali kutoa hoja bungeni ili pori hili lipewe hadhi ya kua mamlaka ili maliasili ziendelee kuhifadhiwa maana vinginevyo ndani ya miaka 15-30 tembo katika pori hili watakua ni histori kabisa.
Eti ndani ya kanda kuna units kama Antipoaching,Tourism,Statistics,Administration na Stores lakini zipo kwa majina utendaji upo kwa bosi Kibonde.Kwakweli huu ni ujinga wakati ndani ya kanda kuna graduates wakutosha bado wanashika bunduki kufanya doria maana according to his legacy if you are not doing patrol then he is not paying you night out allowance!this is comletely non sense to me.
Yani kijiji kama mloka kilichopo jirani na kanda ya matambwe post ndogo ya mtemere hakuna mahusiano mazuri kati ya wafanyakazi wa hifadhini na wanakijiji sasa kwa nini ideology ya Community Based Conservation isitumike katika kurudisha mahusiano?Yani katika uhifadhi hivi ndio vitu vya msingi vya kuzingatia maana uhifadhi ni habari na habari za intelligency zinatoka kwa hawa local people adjacent to the reserve sasa wapi habari zitapatikana kama mahusiano hakuna?
Nimesikitishwa na kutosikia hoja ya Mh.Mchungaji Msigwa ambayo alitaka kuiwasilisha katika kipindi hiki cha bunge lililopita maana nahisi serikali walijua madudu yatakayolipuliwa na watu wangeingia kikaangoni.
Niseme tu sasa taifa linaendelea kumong'onyoka na matabaka yanazidi kuongezeka kwahyo kupanga ni kuchagua kwahiyo napendekeza katika katiba mpya kuwe na utaratibu mzuri ambao kumpata mkuu wa mradi kama huu na miradi mingine mikubwa wapatikane kupitia bungeni na sio katibu mkuu au mkurugenzi wa idara atumie madaraka yake.
Hapa ninapotuma ujumbe huu hali ni mbaya maana watumishiwamepunguziwa posho zao kutoka doria 20 mpaka 10 na hapo kama utakua na kazi za ofisini ndo ujue hulipwi na inasikitisha hata baadhi ya watumishi wakike ambao wanalea wanaishi kwa kutegemea mishahara pekee kitu ambacho nikumnyima mfanyakazi haki yake ya msingi tena kumnyima haki yake kama binaadamu.
Selous bila Kibonde inawezekana kabusa na hata akiwepo inawezekana kama ataweza kufanya kazi kwa mujibu wa kanuni,taratibu na sheria za itumishi wa umma.
Naomba kuwasilisha kwa uchache
 
Back
Top Bottom