Imenikuta hiyo kaka kuna ndugu yangu anapigana root za Jongo, aliwahi nambia kaishia wese akiwa anarudi Vingi, mzee mzima nikajipinda ili ndugu yangu asisumbuke ktk nchi ya mbali, ile hela nilimpatia na nikamwambia kuwa mwezi fulani nitaihitaji ili kukamilisha malengo yangu, ilivofika wakati nnashida ndio ikawa tabu sasa upande wangu, simu haipatikani, mara haipokelewi,,,, nikaja ambiwa kaenda Rwanda na simu yake n mbovu,, baada ya kama miezi 7 ndio nikaja lipwa pesa pungufu kama 1/4 ya pesa nnayomdai..... Kwa kweli kwa bahati mbaya kanifanya niwe na roho ngumu kwani huwa haishiwi shida, nikikumbuka usumbufu ule huwa nami nina shida nyingi zaidi