saadala muaza
Member
- May 12, 2023
- 38
- 38
Mwandishi: Saadala muaza
Lilikuwa ni ziwa lenye uzuri wa ajabu.Uzuri ambao ulipambwa kwa miti mirefu iliyojaa rangi ya kijani.
Pembezoni mwa ziwa hili kulikaliwa na nyasi zilizosambaza mbawa zake na kulipa sura ya peponi ziwa hili.
Katika moja wapo ya miti mizuuri iliyopatikana katika ziwa hili.Kuliishi tumbili mmoja aliyefurahia mazingira haya.
Pembezoni kidoogo mwa ziwa hili alipatikana mamba ambaye naye aliishi kwa kukusanya na kula matunda mazuri yaliyodondoshwa na miti ile.
Mamba akajijengea mazoea ya kutembelea miti ile kila siku kiasi cha kufanya wawe marafiki na tumbili yule ambaye sasa akawa msaada mkubwa kwa rafiki yake kwa kumsaidia kukusanya matunda.Hivyo wakawa ni marafiki wa karibu waliopendana sanaa.
~~ ~~
Siku moja tumbili akamuomba rafiki yake mpendwa mamba akampatie matunda mke wake kama zawadi kutoka kwake kwakuwa matunda ya mti huu yalikuwa matamu sana.
Mke wa mamba alifurahi sana kula matunda yale,matunda ambayo utamu wake hakuwahi kuusikia kutoka kwenye tunda lolote alilowahi kulila.Mamba alimwambie mkewe kuwa matunda haya yanapatika kutoka kwenye mti mkubwa sana ambako rafiki yake kipenzi tumbili ndo huwa anaishi.
Mkewe akamuuliza"je rafiki yako tumbili huwa na kawaida ya kula matunda haya kila siku?" Mamba akajibu ndio
"Waoo mume wangu sijawahi kula matunda yenye utamu wa kiwango hiki.Hebu fikiri ni kwa namna gani moyo wa tumbili huyu ambaye hula kila siku matunda haya utakavyo kuwa mtamu.Mume wangu tafadhali naomba uniletee moyo wa tumbili huyu.Nadhani unaweza."
Mamba alishtushwa sana na taarifa hii "lakini mke wangu huyu tumbili tunaye muongelea hapa ni rafiki yangu tena rafiki kipenzi vipi niweze kumfanyia haya?"
Lakini mke wake akamwambia" we usijali unachopaswa kukifanya ni kumleta tu hapa kisha hayo mengine niachie mimi au unamsukumizia tu kwenye maji kama hajui kuogelea."
Baada ya marumbano ya muda mrefu sana hatimaye mamba akakubali kufanya jambo lile kwa shingo upande.
Siku iliyofuata mamba akamwambia rafiki yake kuwa mke wake amemkaribisha kwa ajili ya chakula cha pamoja.Tumbili alifurahi sana japo aliingiwa kwa kuwa hawezi kuogelea.Lakini mamba akamtoa wasiwasi kwa kumwambia kuwa atambeba mgongoni mwake na hatoweza kabisa kuyagusa maji.
Basi mamba akambeba rafiki yake mgongoni na kisha wakaanza safari huku tumbili akiwa amemshikilia mamba vilivyo kwa hofu ya kudondokea kwenye maji.Wakati wakiwa njiani tumbili akajawa na shauku ya kuujua ukweli ni kivipi mkewe kapendezwa naye mpaka kuomba aende wakapate chakula cha pamoja.
Kwakuwa mamba alimuamini tumbili kama rafiki yake kipenzi basi akamwambia kila kitu kuhusu mazungumzo yake pamoja na mke wake hivyo anampeleka kwa mkewe ili akale moyo wake.
Tumbili kwa haraka haraka akawaza kitu kinachoweza kumsaidia kisha akapata jibu
"Oooh! Rafiki yangu kipenzi.Ungeniambia mapema ili niuchukue moyo wangu maana huwa sitembei nao.Hivyo naomba unirudishe nikauchukue kisha tutampelekea shemeji"
Mamba naye bila kufikiri.Akarudi alikotoka mpaka pale chini ya ule mti mkubwa.Tumbili akaruka na kukwea juu ya ule mti na kisha akapaza sauti na kusema.
"Ewe mamba mjinga.Nilikuchukulia kama rafiki yangu kipenzi lakini umenisaliti.Hivyo sitashuka tena huko na wala sitakuwa na urafiki na wewe kuanzia sasa."
Mamba alisikitika kwa kutambua makosa yake na akarudi kwa mkewe mikono mitupu.

Upvote
3