Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,976
Jamaa mmoja alikuaga akifika bar anaagiza bia tatu tofauti safari castle kili then anatafta meza yenye viti vitatu anakaa nakunywa zile bia moja bada ya nyingine zote tatu nakuondoka. Alirudia hii tabia mara kadhaa ndipo mhudumu wa ile bar akashindwa vumilia ikabid amuulize kwanin anafanya vile kuagiza bia tatu tofauti na kunywa zote? Yule jamaa alimjibu kua waliekeana makubaliano na rafik zake wawili ambao aliishi na kufanya nao kaz kwa pamoja kwamba endapo wangetengana au kuhamishiwa maeneo tofauti bas kila mmoja popote atakapokua akienda bar kunywa bas awanunulie wenzake bia walizokua wanatumia na azinywe ikiwa sehemu yakuwakumbuka nakuenzi undugu au urafik wao kwahiyo hata jamaa nao walikokua walifanya the same.... Siku nyingine tena mambo yalikua tofauti, jamaa aliingia bar nakuagiza bia mbili tu castle na kili, mhudumu alishangaa tena ikabid amuulize kulikoni au kuna mmoja amefariki kati ya wale marafiki zake? Jamaa akamjibu hakuna aliyefariki wote wapo isipokua yeye ndo kaamua kuacha pombe...[emoji16]