Swahiba nimekupata,
Kwanza, bado natetea kabisa kuwa DC kwa Tanzania bado, nafikiri kabisa watanzania bado ule mwamko haujatufikia bado, kama alivyosema mmojawetu hapo juu je ni asilimia ngapi ya watanzania watafaidika? Angalia hao wabongo walio nje Versus Wageni watakao faidika. Tumeongelea tu hiyo social/ community impact na DC, je tumeongelea kuhusu political/ economic deeply? Kwa mifano tu:
AGOA - Hivi jiulize, hii ni kama ile "affirmative action" ya marekani kwa waafrika, tumefaidika nini Africa au Tanzania? Sijasikia hata kampuni moja ya Tanzania ambayo imexport huko marekani at least USD 1million per annum. Sunflag wale wahindi wa Arusha wameitumia hiyo, indigeneous hata mmoja hayupo.
EU- Everything but ...- Hii imemsaaidia nani Africa particulary Tanzania? Ile minofu ya samaki, nani ana-export na nani anafaidika, go deep, na sisi tunabakiziwa mapanki.
China Import Tax Treaty for Africa- Ushuru 0 (ZERO) kwa bidhaa zote zitokazo nchi 25 za Africa including Tanzania. Je how did a common man in Tanzania utilize this?
Kuna treaty nyingi sana ambazo zinaweza kutuondoa katika umasikini, lakini hakuna action inayochukuliwa na serikali aut Taasisi kuhamasisha watu kutumia hizi treaty kuuondoa umasikini kwa kutumia hizi opportunities; nani anafaidika? Je tunayo competition advantage?
We have to workout this first!
Kuhusu China na overseas Chinese:
Mchina yoyote mwenye damu ya mtu wa China anaitwa overseas Chinese, haina lolote kuhusu Uraia. Ukiproove tu wewe una Uchina ndani yake basi wewe ni Overseas Chinese. Hii ya passport ya China hamna kabisa uhusiano huo. Overseas Chinese wako kokote duniani na treatment yao kwa serikali ya China ni special tu wakati unaongelea investment, lakini kuhusu uraia, wako treated sawa sawa na foreigners wengine. Ni Taiwanese (ROC= Repulic Of China) na HOng Kong residents (SAR = Special Administration Region) wako treated na card maalum, lakini si suala la DC. Chinese American au Tanzanian Chinese hawana kabisa hiyo treatment. Wanatumia tu passport zao za respective countries.
Note above: PRC = People's Republic of China (China haitambui ROC, inatambua tu Taiwani ni Kisiwa cha PRC na ni province yake).
Sasa turudi huko kwenye suala letu la DC. Je hawa wachina, wahindi au na wowote wale serikali zao ziliruhusu kwanza DC ndiyo zikaendelea , answer is no. So what happened? Kamuulize mshindo mkeyenge, KANIKI ndiyo rangi yake, hata dobi afanyaje rangi ndiyo hiyo hiyo!
Kwanza nikupe mfano: Wahindi, wachina, wapakistani na wengine kwa nini wametapakaa duniani? Wao walienda nchi za wengine wakaangalia na kustudy sheria za hizo nchi na kuweka makazi, wengine waliangalia loopholes how they can use sheria za nchi hizo na kufanya mambo yao. Wengi wa hawa walikana uraia wao, lakini siyo kuwa damu damu walikana, everything they did for the sake of life. Na hii ni fact dunia nzima. You have to weigh where advantages are then you workout your possibilities. Kwa hiyo kwa wale wahindi, wachina, au pakistanis walioenda marekani kwa kuukana uraia wao (wachina) siyo kuwa walikana ndugu zao, walisacrifice for the sake ya ndugu zao walio nyumbani. Leo hii kuna zaidi ya Wachina 57million as overseas Chinese, na hawa wana roots china, je hiyo western union ina ingiza ngapi kwa siku au mwezi? Je kwa nini sisi tufanikiwe tu hadi ije DC?
Hawa watu wana miamko ya utafutaji, wakienda mahali popote basi huweka nanga na kuanza kufanya kazi. huanzisha community zao, na hufanya mambo yao kama vile wako kwao, na sheria wanazifuata.
Swahiba, ona India na China, biashara zao kwenda marekani au EU kuna quota system, MFN (most favoured nation status), au tax. Sisi tunaambiwa tu-export tunavyoweza hata hivyo hatuna cha ku export. Hata kutumia huo unafuu wa AGOA, EU, China, kuwaita wawekezaji, bado tuko pale pale! What we are lacking? We are lacking Either the revolution theory or we do not know if we are poor.