Bwana Masanja,Honestly, mi naomba unipe sababu kubwa kwa nini unapinga uraia wa nchi mbili zaidi ya hizi non-existent reasons za maslahi ya taifa? ambazo wanasiasa wamezitumia miaka yote kutukandimiza kwenye lindi la umaskini? Maslahi ya taifa ni yapi? nani anayasimamia? Hao wageni unaowasema kuja kutuibia, kama ni kuja walishakuja na kuiba na wanaendelea kuiba saana tuu. Mimi ninachokiona humu ni kwamba wenye nacho hawataki wengine wapate. Acheni watu watafute pande zote za dunia from Belize to Singapore.
Bwana kwangu mimi as long as kitu kitamsaidia mtanzania mwenzangu hata kama hakitanisaidia, Tuache kimsaidie! Tuache unafiki wa kuimba maslahi ya taifa kumbe ni maslahi ya Lowassa na wenzake wachache.
Dual Citizenship? Labda Niulize tu ..
Kwani hao wanaodai hilo si walikuwa Watanzania? Vipi wakaukataa huo Utanzania sasa wanautaka tena?
Kuna mtu kataja UZALENDO ... i think thats key.. kama upo, basi huhitaji kuwa na dual citizenship kuendelea kuipenda nchi yako. Na kama uliamua kuwa Mwingereza kwa sababu za kuhangaikia maisha, vizuri, nchi yako ya damu si bado ipo, haikukatazi kuichangia kwa njia zote za kimaendeleo. Hicho wengine wanafanya, bila duo citizenry.
Karibuni Wazalendo!
Kisura, mbona una jazba hivyo leo...kulikoni...hukulala vizuri nini? Uko mkali kweli leo mpaka wanitisha hata kukusalimia....
Bwana Masanja,
Labda ungeanza kwa kunipa sababu za kunieleza faida za duo citizenship zaidi ya kuwafaidisha wasio watanzania kwa kuwapa citizenship by naturalization.
Watanzania tunapenda mterememko and are very good at finding easy way out/in.
Richard,acha jazba zako,issue sio kuwa na pass mbili tatu au nne,issue ni URAIA wa nchi mbili
Nisalimie tu, usiogope. Ni suala la "duo" tu ndio lanifanya nisilale vizuri.
In my opinion, advantages of Dual Citizenship are purely socio-economics. The privilege aims to broadening a relationship between economic activities and social life. The Dual Citizenship proposal for Tanzania is no difference. It aims to broadening our countrys economic activities and social life bases by promoting trade and investment between the dual citizens two respective countries.
Kwanini kuwe na uoga wa wageni kufaidika na D.C.? Kama swala la wageni kutumia hii privilege kuchuma mali zetu, basi pengine itatupa changamoto ya kuamka na ku-protect hizo mali zetu ambazo zimekuwa zikiibiwa for years anyway. Kama hao wageni watakuja na kuwekeza bongo, si ndio mwanzo wa ajira kuongezeka? Mimi nafikiri pengine muda umefika wa kuacha kuogopa wageni, kwa sababu utake usitake watamiminika tu. D.C. ni sehemu ya Global movement . itakuja tu sooner or later.
Ni kweli tunapenda mteremko. Na ndio maana bado mpaka leo tunaishi maisha ya kunyonyana. Kwa hiyo pengine hiyo D.C. inaweza kusaidia kuacha hiyo tabia ya mteremko, kwa sababu tutapata njia mbalimbali za ku-exercise options zetu. Bila ya kusahau, ujio wa wageni utatupa changamoto ya ku-hussle.
Damn! if we haven't yet figured out how to protect our resources and interests then we are slow as hell....
Unadhani tutapopata mbinu za kuPROTECT? watakuwa wamebakiza kitu. Hiyo ajira ndio itaongezeka, bado kuna mifano mingi ya investors,mfano wachina, wahindi, kuja na watu wao kwenye kazi zinazoweza kufanywa na wazalendo, na hii itatoa mwanya zaidi.
Damn! if we haven't yet figured out how to protect our resources and interests then we are slow as hell....
Tena kuna dozens of evidence to support that...the more reasons why Tanzania does not need dual citizenship, not now!
Tuacheni sera za uoga jamani. Unafikiri hao wageni wameanza leo kuchukua hizo mali zetu? Nina uhakika tunaamka kwa speed mzuri. JF ni mmoja wa mifano halisi kwa jinsi tunavyoamka. A decade ago Watz wengi bado walikuwa hawajagundua kwamba internet inaweza kuwa dimba la kubadilishana mawazo. Leo hii forums na blogs kila kona. Kwa hiyo kwa jinsi hii wananchi, pamoja na serikali, wanaweza kuunda njia haminifu za control what what goes out and comes in the country. Ninaamini siku za usoni wananchi wengi watakuwa na uwezo wa kunyooshea vidole mambo ambayo yatakuwa yanaashiria ubadhilifu wa mali zetu.
Kuhusu wageni kuja na watu wao, ukweli ni kwamba hawawezi kuja na entire workforce. Bado watahitaji manpower ya wazawa. Sana sana huwa wanakuja na wataalam na management zao, lakini entire subordinate inajazwa na wazawa. Sasa huoni kuwa hiyo ni ongezeko la ajira?
Sera za uoga ndio zinatufanya mpaka leo hii hatuwezi kupaza sauti zetu kwa nguvu enough kumng'oa kiongozi mbovu. Tunahofia wageni kuja kutuibia, lakini ukweli ni kwamba ni sisi wenyewe ndio tutaongoza kwa kuibiana, kama tunavyofanya sasa. Siku zote kikulacho ki miongoni mwako!!!
Kisura, wewe unaliangalia hili suala katika mtazamo wa uwekezaji/ biashara mno ndio maana Unalipinga kwa hali na mali.
Ila hoja yenye nguvu ni hii ya kifamilia. Nimemsikiliza Mwanakijiji, na yeye inaelekea anaikubali hoja hii ingawa yeye hakuipanua (no pun intended) kujumuisha na watoto. Yeye kaishia kwenye mke na mume tu. Hii hoja inasimama peke yake!